Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKINUKUU BIBLIA, KORANI au kamaSUTRA kwa MTU asiyeamini MUNGU!

>> Wednesday, April 30, 2008

Binadamu hupenda kunukuu watu, vitabu, matukio, ..... katika kujazia uzito au hata kuhalalisha kitendo au mtazamo wa mlolomo wao.


Binadamu , kirahisi, husahau wengine hawafikirii wala kuamini ukweli wao ni ukweli hata kama unaitwa sayansi wakati wanamnukuu Einstein kuwa E=mc2

Swali:

  • Unakumbuka kuna ambao E=mc2 ni= na ALbaMU mpya ya Mariah Carey na hakuna uhusiano wowote na Fizikia(Phisics)?
Nachojaribu kunong'ona ni:
....Unaponukuu mwingine asichoamini , unaweza ukawa unajipotezea muda.

Ukijikumbusha nukuu za mtoto.....
.....LImwanaMKE LAKO au LIBWANA LAKO ufikirialo kuwa ni zuri na lina roho nzuri, na ni tamutamu kama lawalawa nyama, linaweza kumliza mtoto mdogo akalia kama vile kaumwa na manyigu , kutokana na kumuogopesha MTOTO, kwa sababu kwa nukuu za mtoto, huliona hilo LImTU LAKO kuwa lina sura kama Nundu na meno kama Ngiri.


Ni rahisi kusahau kuwa kuna vitu vingi mtu umejifunza kuviogopa na hukuzaliwa unaviogopa, kitu ambacho mwenzio anaweza akawa bado hajajifunza kuviogopa na haogopi kama wewe.


Sasaaaa......

....ukimtishia asiyeamini MUNGU, maswala ya MUNGU , anaweza akamtukania Mungu wako , halafu ukajikuta umempiga ngwala, mtama au hata kuMKOLIMBA , kabla hauja MSaddam Hussein.

Lakini naamini kuwa....
......baada ya UBONGO WAKO kuamini kitu, tafsiri na wapi unanukuu viushahidi vyako au vikupovyavyo roho kuwa uko upande sahihi, HUATHIRIKA.

Inawezekana umeathiriwa na ELIMU.
Si ndio maana unanukuu vinavyotoka vitabuni ?

Inawezekana umeathiriwa na dini.
Si ndio maana karibu kila jambo utanukuu VITABU vya DINI ,mapenzi au hasira za MUNGU?

Inawezekana umeaathirika na utamaduni fulani.
Si ndio maana kuna mahali unanukuu mpaka wacheza Sindimba matiti nje, pale AIRPORT wakati Raisi wa nchi fulani ya Kiafrika kawasili,kuwa wako uchi na wafanyacho si utamaduni ASILI wa KIAFRIKA, iLA, unaamini pamba itokayo India inatengeneza nguo halisi za Kiafrika?

DUH!

Sehemu unanukuu, inaweza ikawa ni kama ujumbe uupatao kwa kuangalia sanamu.
Sentensi uitoayo kwenye sanamu ,inaweza kutowakilisha kwa mwingine ilichowasilisha kwako.

Swali:
  • Sanamu ni nini?
  • Sanamu huwakilisha nini kwako?
  • Unajua inawezekana kila mtu ANAABUDU sanamu?
  • Mwalimu asimamaye mbele yako darasani, na kuondoka bila wewe kujifunza au kuelewa kitu , hawezi tafsirika kama sanamu liwakilishalo kitu tu chenye jina MWALIMU?
Kuna atakayesema sanamu huwa alifanyi kitu, linawakilisha tu kaujumbe kawakilishwako na sanamu.


Lakini...
...wako watakao kumbuka, sanamu linaweza kukuangukia na kukuvunja nanihii!

Naacha basi kukuzingua!
Usitishike Nawaza tu hapa!

Karibu tena MAWAZONI lakini!

Pata basi TAP DANCE kutoka kwa Savion Glover

Au....

Mcheki tu Maraya Keri katika wimbo Touch my Body kutoka albamu E=mc2

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP