Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STORI KUHUSU WENGINE WAFANYAVYO NGONO!

>> Thursday, April 03, 2008

Kuna watu wengi ingawa ni vigumu kukiri, stori za ngono zinawafanya wawewasikilivu na ndizo hata huku mtandaoni ziwawekazo bize.

Nafikiri hawa watu bomba tu!

Ni ukweli stori hizi zinamvuto wake, halafu hazihitaji uwe profesa kuelewa jamaa aliguna.

Lakini......

....mara nyingi watafutao na wanogewao na stori hizi za mchezo wa baba na mama, hupenda kufuatilia WENGINE wanafanyaje huu MCHEZO wa BABA NA MAMA na hawapendi hata kidogo hizi stori zifuatiliwazo na wafualiazo ziwe zinawahusu WAO BINAFSI.

Mdau apendaye kusikia twende tukamchungulie jirani wakati anajinoma, huwa hapendi kusikia kuwa jamaa walimchungulia akinanihii.

NI STORI NA PICHA ZA WENGINE wakifanya au kuzungumzia NGONO , zinogazo masikioni mwa wengi.


Lakini....
.......inawezekana kabisa kuwa wakati ulinogewa, uko katikati ya mnogo na hata baada ya kufaidi, ukashindwa kukumbuka hatua au hata sekunde ulizopitia katika kujaribu kuhamasisha utamu kitu kifanyacho stori yako ulavyo nyama ya bata, ikawa na mapungufu kuzidi ya yule aliyeshuhudia ukinywa uji .

......inawezekana kabisa kuwa kama uko makini katika kusikilizia ladha ya nanihii, ukashindwa kujua au kusikia kuwa kuna mwizi sebuleni.

Swali:

  • Wakati unafanya mtihani, ushawahi kukumbushwa umebakiza dakika ngapi za mtihani ingawa una saa mkononi ?
  • Unafikiri ni kwanini muda unakimbia ukiwa katika mtihani ,mpaka unakiri hata hujui muda umeenda wapi lakini una nafasi ya kuhesabu nzi waliokutembelea mezani pale mgahawani wakati unamsubi yule ... atokee?
Nakubali kuna watu wapendao stori zao za karibu kila kitu zijulikane na zisimuliwe.
Najua wapo pia ambao mpaka wanajitungia stori na kuziweka kijiweni ili ijulikane kuwa jana walikula mtori au makande.

Lakini...
... stori nzuri na ipendwayo na wengi siyo ile isimuliwayo na mtenda jambo.

Stori tamu ni ile jamaa wameistukia na ile wewe unaisikiliza na kuitafuta kisiri ukijifanya haikuvutii.

Bila kusahau......
...... tamaduni zetu za kuficha mambo kibao na kutofundishana mambo fulani, yanatuponza watu kibao kuanza kujitafutia ufundi wa kufaidi utamu katika stori na hata zile picha ambazo unajifanya hutaki kuziangalia kama kuna watu wanakutumbulia macho.

Tamaduni zetu zinatuficha mengi tu ambayo kama tungefundishwa na yangekuwawazi, hata yasingekuwa yanatuogopesha, kutuvutia au hata kutupotezea muda wa kusubiria BUNGENI waliahidi nini.

Si unakumbuka baadhi ya mambo tamaduni zetu inayofanya ni siri kama:
  • Uchawi
  • Ngono
  • Nini ufanye ufanikiwe kama mimi au yule....
  • na.......nk.
AU?

Swali:

  • Hujawahi kuwa msikilivu wakati umestukia jamaa wanaongelea kitu ambacho unajua hawataki usikie?
DUH!
Naacha basi!

Lakini kumbuka, kutokana na utafiti HUU HAPA, binadamu anatoshelezwa MAHITAJI YAKE YA NGONO ndani ya dakika tatu mpaka kumi na tatu na SI LAZIMA IWE milele, kama mlaji anajua KULA na MWENZIYE.

DUH!
Ngoja nikuache na huu wimbo baadhi ya wanaume wasemao ndio usemao ukweli kuhusu...
hebu cheki:

Ngojea nirudie ustaarabu basi!
Tulia na MARVIN GAYE akikuimbia kile kitu LETS GET IT ON.

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Simon Kitururu 9:36 am  
This comment has been removed by the author.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP