Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TANGAZO kwa WADAU walioko HELSINKI !

>> Friday, April 11, 2008

UNAKARIBISHWA katika ile PATI YA WAAFRIKA yaKILA mwezi
ndani ya HELSINKI.

Tarehe: 12.4.08

Saa: 21:00 mpaka 04.00

Mahali:Ravintola Kaisaniemi

Anuani ya sehemusehemu: Kaisaniementie 6

Kiingilio: 5 Euro

Kutunziwa Jacket: 2 Euro

DJS: EDDO the MAN akiwa na ALIKO aka Altunes














Karibu
Mmoja !Karibu Wote!
Kwa habari zaidi nenda
: www.africannight.org

DUH!
Haka kawimbo kamtajako mende aka Kaka ROACH (Kakaroach in meh petty coat), kamenikaa kweli kichwani mwangu leo....


Naona nimemzidisha LORD KITCH !

DUH!

Usisahau kuwa pati hii mpaka Msondo Ngoma ni mbele kwa mbele.
Basi tulia na mwanadada nimzimiaye aka Lady Jaydee akikuambia USIUSEME MOYO

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 10:37 am  

Mzee Simon,ni vizuri kuwaona waafrika wamekusanyika pamoja na kucheka kama kaka na dada.Sasa Mzee Simon naomba kukuuliza katika mziki huo mnapiga nyimba za iana gani?
Kwasababu kuna zile nyimbo za kutulewesha sisi waafrika,nyimbo ambazo zinaishia mwisho wa pua.Naamini kabisa MWAFRIKA ANAPASWA KUSILIZA NYIMBO ZA HISIA (ROOTS REGGAE TU)NYIMBO ZA HISIA ZINAKUAAMUSHA NA KUAZISHA CHANGAMOTO YA THE BLACKSTARLINER,ZITAWAFANYA MUAANZE KURUDI AFRIKA KWANI SISI TUTAKUWA BAHARINI KUWAPOKEA NA KUWAKARIBISHA NYUMBANI.

AMANI.

RASTA HAPA.

Simon Kitururu 1:07 pm  

@Rasta:Mimi sihusiki na pati hiyo.SOma vizuri TANGAZo utastukia jina langu halipo. Nafikiri ukisoma vizuri tena, utaona Djs ni Aliko na Eddo.


Hivi ROOTS REGGAE ndio nyimbo za kiafrika tu?Kama ni kweli Roots Reggae ndio muziki wa kiafrika pekee, basi Waafrika asilimia kubwa duniani hawajawahi kusikia nyimbo za kiafrika.

Wewe kama Rasta , na mfuatilia historia . Kumbuka Black star line ilianzishwa 1919.

Marcus Garvey aliyeanzisha Black star line alikufa 1940

Roots Reggae ilianza miaka ya 1970s baada ya rock steady

Hata waanzilishi wa Black star line , inawezekana hawakuwahi kusikiliza ROOTS Reggae.Na nauhakika wako ambao hata baada ya kusikiliza hawakuwa impressed.

Kwa hiyo ukifuatilia vizuri historia ya Roots Reggae na Blackstarliner, unaweza kugundua kuna uwezekano kuwa hata Marcus Garvey hajawahi kujua Roots Reggae ni nini.

Sioni kwanini mtu mwingine akisikia Roots Reggae ndio atake kurudi Africa. Nawajua watu kibao ambao wakisikiliza BONGO FLAVA au NDOMBOLO ya SOLO ndio wanajisikia labda wamezidisha kukaa nje ya Africa na kufanya mpango wa kurudi.

Na wengi warudio , hurudi kwa ndege na hawawazii meli kama ilivyo kuwa Black star line.

Nakuelewa lakini!
Nanaheshimu angle yako yakuona mambo.
Amani Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP