Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WASHINDI ndio huandika HISTORIA

>> Wednesday, April 09, 2008

Inasemekana kuwa kama hujui historia yako ni rahisi kuathirika, hasa katika idara ya kujiamini.

Lakini...
....wengi wapendao kuongelea historia, ni wale wafaidikao na historia hiyo kujulikana.

Historia yako ya kwamba tokea enzi za mababu mna kifafa na kuwa mnachelewa kuacha kujikojolea, unaweza usiishabikie watu wajue.

Wazungu ambao kwa muda fulani wamefanikiwa kutawala sehemu kadhaa duniani, hawakawii kukusimulia Napoleoni alikuwa nani na hata kukuhakikishia jinsi gani YESU alikuwa anamacho ya blue na nywele blondi.

Mshindi huandika historia.
Aliyeshindwa , akiandika historia inaweza ikakosa bajeti ya kuchapisha vitabu hivyo.

Kizazi cha aliyeshindwa kiko hatarini kukosa kusikika au hata kikisikika na kuwa na kinyongo, kujikuta hakijiamini hata pale ambapo kikojuu ya jambo.

Mambo yazungukayo kizazi kisichoandika historia yanaweza kusababisha kizazi chake kusikiliza maoni ya kizazi kilichoshinda hata yakiwa yakijinga.

Swali:

  • Hivi unafikiri kwanini kula nguruwe inaonekana kawaida kuliko kula mbwa maeneo hata bila ya mtu kuwa na ushahidi wa ubaya wa nyama ya mbwa?
  • Ushawahi kujiuliza kwanini bikini ni vazi mpaka sehemu za baridi kama Ulaya jua likitoka, lakini vibwaya watu haohao wanaweza kukuambia ni kutembea uchi hata kama unaishi nchi isiyo na uhaba wa jua?

  • Msomi haja kukuongelesha ung'eng'e ingawa wote mnaongea kiswahili?


Washindi hutawala.
Lakini hakuna kitu kiitwacho kutawala milele.

Washindi watakuambia wanajua hata ndugu zako wangapi walikufa na KIPINDUPINDU , wakati nyie wenyewe mkashindwa kubisha idadi mpewayo ya kuna vichaa wangapi walao jalalani hapo mjini.

Lakini.....
...kumbuka tulioshindwa bado tuko hai.


Na....
......kumbuka, washindi si lazima waandike ukweli wa jinsi gani walishinda.
Inawezekana kabisa kushinda walikokusimulia kulikuwa na tafsiri tofauti na kushinda kwa uliye ambiwa alishindwa.

Kama tafsiri ya kushinda ni kwamba kapata alichokitaka.
Inawezekana mkoloni tujisifiaye kuwa tulimshinda akawa bado anatushinda.


Swali:

  • Kwani mshindi ni lazima akuambie au kukuonyesha amekushinda wakati bado anapata?
  • Unauhakika aliyeshindwa hakupata atakacho?
  • Hivi kushinda ni nini?

DUH!

HISTORIA YA ALIYESHINDWA inaandikika lakini.

UKIKUMBUKA kuwa umeshindwa na ukawa na uchungu na kushindwa , unanafasi ya kujiandaa kushinda.

Swali:
  • Umeshindwa?
Naacha basi!

Jaribu kukumbuka haka kaujumbe kuhusu UKIMWI, hata kama inasemekana kuwa idadi ya Wasauzi Afrika inaongezeka kuliko kupungua pamoja na mdudu kuwa hachezi mbali na wewe ukionja nanihii Usauzi.
AU?


DUH!
Najua wengine leo walikuwa wanataka atakacho JAMESY P usiku wa leo...

KUWA MUANGALIFU!

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 8:10 am  

Mzee Simon,naamini kabisa HISTORIA INA PANDE MBILI.KWANZA WALE WALIOFANIKISHA NA WALE WALIOSHINDWA KUFANIKISHA MAMBO.

KWA MFANO HISTORIA YA JUMUWATA ITAANDIKWA NA ITABAKI MILELE.WALE WALIOLETA CHANGAMOTO JUU YA JUMUWATA MAJINA YAO YATABAKI KATIKA KITABU CHA HISTORIA PAMOJA NA MAJINA YA VIONGOZI WA JUMUWATA NA KILA KIONGOZI KAZI YAKE ITACHAMBULIWA NA KUANDIKWA.

RASTA HAPA.

Anonymous 8:10 am  

Mzee Simon,naamini kabisa HISTORIA INA PANDE MBILI.KWANZA WALE WALIOFANIKISHA NA WALE WALIOSHINDWA KUFANIKISHA MAMBO.

KWA MFANO HISTORIA YA JUMUWATA ITAANDIKWA NA ITABAKI MILELE.WALE WALIOLETA CHANGAMOTO JUU YA JUMUWATA MAJINA YAO YATABAKI KATIKA KITABU CHA HISTORIA PAMOJA NA MAJINA YA VIONGOZI WA JUMUWATA NA KILA KIONGOZI KAZI YAKE ITACHAMBULIWA NA KUANDIKWA.

RASTA HAPA.

Simon Kitururu 9:41 am  

@Rasta:Nakubaliana kabisa

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP