Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HUKUJUA umeshaMTEMA yule KIPENZI , au UNAHURUMA tu?

>> Wednesday, April 09, 2008

Watu wabishi tu!
Penzi hufa.

Watu mara nyingine si wabishi!
Wanaogopa tu walivyotishwa na dini zao,ndugu zako au zake, mganga wa kienyeji au hata kibano cha mazoea, kukubali kuwa penzi lilishakufa mwaka juzi.

Si lazima mpaka uwashwe ndio ustukie yule kipenda roho hakufikishi katika mkuno wa pendo.

Pendo halilazimishiki.

DUH!

Pendo nishai!
Unaweza kupenda mpaka ukapofuka na kushindwa kujua ulishaachika moyoni mwa mpendwa mpenzi .

Pendo nishai!
Unaweza ukapendwa mpaka ukafanikiwa kutokuwa na bidii ya kuonyesha penzi kutoka na kutoshuhudia malipo ya penzi.

Si unajua!
Unaweza kupendwa mpaka hata usipojiangaisha kushughulikia palilizi la pendo, dagaa uzipendazo , utapikiwa tu.

Pendo nishai!
Linaweza kufa halafu ukakosa staili ya kumtema akufikiriaye wewe bado unampenda.

Swali:

  • Nani kakuambia kuna staili moja ya kumstua mpenzi kuwa penzi limekufa?
  • Unauhakika kuwa nanihino bado anakupenda kama ufikiriavyo?

Samahani kwa kukuzingua!
Unajua tena, niko mawazoni tu!

KARIBU TENA na Jumatano njema!
Burudika na LORD Kitchener ,kama ma-soca/calypso yanapanda kama MIMI....akija na SUGAR BUM BUM

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 6:12 pm  

Mzee Katibu,napatikana hapa
http://rundugai.blogspot.com/

Rasta Hapa.

Simon Kitururu 4:47 pm  

@Rasta:Nimekuona pale Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP