LABDA hutaki kuona MAJINI,MIZIMU, NDONDOCHA au hata KIDONDANDUGU!
>> Tuesday, April 15, 2008
SWALI:
- Unataka kuona au KUTOSIKIA nini LEO?
Lakini...
....mwingine anaweza akawa na uhakika kuwa tunaona na kusikia mambo fulani kwa sababu tunawekea umuhimu mambo hayo au hata kuyatafuta kwa kutumia, jicho sikio au hata akili.
Inawezekana hata tukawa tunachagua jinsi ya kuona au kusikia jambo , ndio maana muziki mzuri kwangu , kwako makelele , na kitu kizuri kwangu, kwako kina sura mbaya na kinanuka kikwapa.
DUH!
Kutokana na utafiti mbalimbali, watu huona mpaka mizimu , majini au hata ndondocha kwa sababu tu walishaambiwa kuwa katika makaburi hayo, saa sita usiku , kuna jini na mizimu inacheza sindimba.
Hebu angalia hiki kideo uone jinsi kirahisi unavyoweza kutoona kitu mbele yako kama hutafuti kukiona....
Kisayansi pia wanadai kuwa sehemu iliyo na cabon monoxide nyingi, nguvu za elektro magneti kubwa, zinaweza kuingiliana na ufanyaji kazi wa ubongo, na kukukusababisha uanze kuhalusineti au kuona vitu ambavyo havipo.
Lakini....
.....kikubwa kikufanyacho uone au kusikia kile kitu, ukiondoa kuwa unataka kukiona au kusikia kutokana na yaliyojengeka akilini mwako tokea uzaliwe mpaka sekunde hii ya kukipigia chabo, ni kwa sababu jamaa washakuambia ukifika Makambako, usile nyama, kwa sababu zinaweza kuwa ni za kunguru.
Hebu cheki kideo hiki pia....
Unafikiri bila kusimuliwa kwenye kideo kuna nini, ungeona MBILIKIMO au WATOTO wanacheza MPIRA wa MIGUU?
Lakini....
...inawezekana unaona au kusikia pia vitu ambavyo vinaonekana na kusikika kutokana na kuwa vinaonekana na kusikika.
AU?
SIKU NJEMA!
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
yep.
yote umemaliza wewe bro sina la kusema..hicho kichwa sio urefu wa rasta tuu yaani una akili ndugu yangu.
lulu
@Lulu: Asante sana kwa kunitembelea na kunifagilia Dada!
Simon,kweli wewe mawazoni, duh kaka yangu unachimba sana kibook!!!!!asante sana,usichelewe kutulea habri zingine za kusisimua kama hizi!DUH
you see ...what I n I haffi deal with daily! guidance and protection against all evil
@Aliko:I &I haffi got to deal wit dat
Post a Comment