Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAUHAKIKA unakasirikia KILICHO KUKASIRISHA?

>> Thursday, April 03, 2008

Si siri, wote tunakasirika mara kadhaa kabla hatujafa hapo baadaye!

AU?

Kukasirika bomba la kazi!

Kukasirika ni shughuli ikuchoshayo wewe kuliko yule kwa sababu inabidi wewe ndio ukasirikie kitu/vitu, mtu/watu kabla hujajikasikia mwenyewe !Hakuna ujanja wa kumuajiri mtu afanye kazi yako ya kukasirika.

Kumbuka pia , kukasirika kunasababisha utumie misuli kadhaa ikiwepo ya kukunja ndita na hata kusababisha uvuje machozi au hata.....

KAZI KWELI KWELI!

Swali:

  • Mara ya mwisho ulimnunia nani?
  • Ushawahi kujiangalia kwenye kioo wakati umenuna?
  • Hivi mkao wakununa wakati una hasira na wakati unahuzuni ni sawa?

Ukikasirika , unaweza ukajikuta unakasirishwa na kikufurahishacho.
Tatizo moja, linaweza kusababisha uone matatizo pasipo tatizo.

Unaweza kabisa kunikasirikia kwa sababu huko ulikotoka wamekukasirisha.
Unaweza ninunia kwa sababu yule nanihii kakukasirisha kule nanihii halafu umeshindwa kumkabili yule na kunikasirikia mimi kwa sababu nyuma ya akili yako inakuambia kuwa mimi ni kibonde.

Hasira kama matatizo, mengine tunajitafutia siye wenyewe.

Unawezakubisha!

Lakini ...
....matatizo mengine ambayo mpaka masikio yamezoea kuyasikia, kama vile umasikini, yaweza kuwa nimejitakia.

Utamu wa kukasirika ni kwamba, ukiwa masikini hata kwa kujitakia kutokana na kutofanya ulichojua ufanye kujikwamua au tajiri ,unaweza ukawa huru kumkasirikia TAJIRI ,MASIKINI mwenzako,JAKAYA KIKWETE, MWAI KIBAKI,GEORGE BUSH na hata MAMA TERESA.

Matajiri wakikasirika hawakawii kukuonyesha hasira zao mikono kiunoni, na sio tu kwa sababu wamestukia huna ujanja na mwisho wa siku inabidi ujipendekeze. Na siye watazamaji, hatukawii kumkasirikia tajiri kwa kitendo chake cha kumkasirikia masikini kirahisi , hata kama ni kweli masikini alikasirisha.


Lakini...

..kukasirika kama kulia, husaidia baadhi ya watu kupitisha siku au hata kujisikia nafuu.

Swali:
  • Hivi umenuna eeh?
  • Ushawahi kujisikia vizuri baada ya kumaliza mkasiriko?
Naacha Basi!
SIKU NJEMA!

Tulia na CEE LO GREEN , mdau aliye kuwa GOODIE MOB na sasa hivi GNARLS BARKLEY ..

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 3:52 am  

Na hapo umeneena rafiki. Saa hii nilikuwa nimekasirika lakini niliposoma kurasa hii yako, nimecheka juu hata sijui nini hicho kilikuwa cha ni kasiricha. Siku Njema..Pole swahili changu sio kizuri sana lakini mimi Mkenya :-)

Simon Kitururu 5:25 am  

@anony:Asante kwa kunitembelea!Kiswahili chako bomba tu Mkuu!

Anonymous 7:37 am  

Mzee Simon,
naamini kabisa kukasirika si tabia.Kwa mfano JUMUWATA ilipofikia na ukimya wa viongozi WA JUMUWATA.Naamini kabisa ukikipenda kitu then usione maendeleo mwishoe hukasirika na kujitoa na kubakia kuchangia kama navyofanya.

Rasta hapa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP