Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

USHAWAHI KUKANA KUWA WEWE si MUISLAMU?

>> Tuesday, April 01, 2008

Samahani!
Nilikuwa nataka kuuliza ;USHAWAHI KUKANA WEWE si mkristo?

Kukana kitu ni kukubali kitu fulani ili kukubalika au hata kutengeneza msimamo ujengao mwonekano wako uathirio kukubalika.

Kukubalika ni kitu watu wengi huanza kukifanyiakazi toka utotoni.
Unaweza ukastukia mtoto kashaanza mpaka kuhonga peremende kwa watoto fulani, atakao kuchezanao ili wamkubali katika kikundi chao!

Kwa wengi, piga ua, ujanja ni kukubalika .

Iwe kazini , mtaani, shuleni au hata pale gizani kwenye ile kona upatapo mahitaji yako ya kisiri ambayo hutaki tujue, kwa wengi wanakuwa na amani moyoni wakijua wanakubalika.

Swali:

  • Unauhakika hufuati hiyo dini kwa sababu ya kujipendekeza ukubalike na MWENYEZI MUNGU?

AU?

Kama kawaida , maswala ya kukubalika , yanakuwa matamu ukiingiza udini.

DINI ni KITU cha AJABU sana!


Dini , humfanya mjanja akubali kula muhogo wa kuchemsha , hata kama anachotaka na alicho nauwezo wa kula ni vitumbua au mkate fulani.

SWALI:
  • Ushajiuliza ni kwanini BARACK HUSSEIN OBAMA anajieleza sana kuwa yeye si muislamu katika kinyang'anyiro cha kazi ambayo haihitaji dini kuifanya?
  • Hivi wewe , kisiri , unafikiri ni akina nani kati ya WAKRISTO , WAISLAMU , Wasayantoji ,... watakao kwenda MBINGUNI?
  • Unajua maana ya jina lako ,na lina maana gani ambayo inagusa dini yako unayoifanyia kazi kila siku kuiamini ?
  • Hivi jina lako lina maana kubwa zaidi izidiyo kuwa uitwapo hilo jina unaitika?
Kuna watu ambao tuna bahati mbaya kimajina!

Mtu akikuuliza tu jina , anakuwa anafikiri anajua tayari kwa uhakika kuwa wewe ni dini gani.
Watu kibao wanaweza wakaanza kuongea au hata kufanya matendo tofauti wakishastukia jina lako tu, kwa kudhani washafahamu maadili yako.

Utakuta stori za kiti moto zinakufa wakistukia wewe muislamu bila kujali kuwa siku nzima walikuwa wanaongea na kukaa pembeni ya msabato ambaye naye nyama ya nguruwe ni haramu vilevile.

Kuna kipindi nilikuwa mitaa fulani Zanzibar, ikabidi nitamani kujiita jina tofauti kutokana na kuhisi nakosa mambo fulani muhimu kama;kuaminika, demu, na ..... kutokana na jina langu kukaa kikiristokristo.

Swali:
  • Baada ya muda wa dakika ngapi kupita ,ndio unaanza kujiuliza uongeaye naye ni dini gani?
  • Kwa wewe Mkristo usiye jiita mlokole, unafikiri MLOKOLE anafikiri mtakuwa kijiwe kimoja MBINGUNI?
Wote kinamna tunataka kukubalika.
Ila.....
...... UJANJA NI KUJIKUBALI MWENYEWE.

Naamini ukijikubali ni rahisi kuhimili pale watu wasipotaka kukukubali.

Lakini...
...swala la kujikubali ni gumu, kutokana naudhaifu wa ubinadamu usababishao kufikiri nanii akutoleaye macho kwa sababu anaitwa MCHUNGAJI , Shekhe, Rabai,.........na.....anajuazaidi naasemacho ndio ukweli mtupu bila dosari kiduchu.

Wengine wanafikia mpaka kufanya operesheni za kukata sehemu za uume ili kujikubali kuwa alizaliwa kimakosa kama mwanaume.

Tusisahau wajichubuao na.. katika maswala ya kujikubali.

TATIZO la dini zetu ambazo wote huziita ni za amani, zina uwezo mkubwa sana wa kutukumbusha na kutufunza kuwa wewe ni tofauti na mimi.

DINI hizi kadhaa , hupenda kutuhakikishia kuwa wewe ni sahihi na mimi ni nimepotea.:-(

Hakuna apendaye kuwa katika upande nishai ,usiojua wafanyalo , uendao motoni,...matokeo yake ni rahisi kujikuta unajitetea sana na kutetea sana upande wako wa dini ya KIGAGAGIGIKOKO.

Usipojiamini, ukajikuta wewe MSAYANTOLOJI umezungukwa na wa-MENONAITI, unaweza kujifanya unawaelewa au hata kukana kuwa wewe si MSAYANTOLOJI , na kule nanihii unakwenda kwababu kunabustani au Maktaba nzuri na sio kwa sababu ya mahitaji yako ya kidini.

Swali:
  • Unakumbuka unavyokuwa huru kusema dini fulani wanachemsha ukiwa na wadau wako mfuatao dini moja ya KILAJI?
  • Ushawahi kutaka kukana kuwa wewe si wewe, na jamaa waliokutambua ukadai wanakufananisha tu?
  • Unakumbuka lakini, hakuna anayefeli mtihani asiye na sababu ya kwanini kafeli na sio kosa lake?
  • Hivi unauhakika usingezaliwa katika dini hiyo au kukutananayo pale ulipokwenda kushoto badala ya kulia ambako wenzako hawakuenda, ungefikiri dini hiyo ndiyo ya kweli ?

BASI BWANA!
Naacha !
Twende SOUTH AFRIKA tupate hii kitu Uya kwini ka rose remix

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP