Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

CHUPI, BAISKELI, BIRINGANYA, ......Majina ya sehemu ZA SIRI,Harage MOJA au PIA neno lisilo BISKUTI.

>> Tuesday, April 22, 2008

Naheshimu neno!

Toto la binadamu likizaliwa, baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza ,ni neno baba au mama linatamkwaje.

Jitu zima likishakua , baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza katika lugha fulani mpya, ni matusi, kutukana au kama halina aibu kama mimi, litajifunza kwanza mpaka majina ya sehemu za siri kwa Kichina.

Lakini....
....inasemekana kuna maneno, kubwa zima halitakiwi lisikike limesema kama linataka kuonekana lina busara au kama linataka kuheshimika.

MANENO ni kitu cha ajabu sana!

Unaweza ukajikuta umeyatumia kumwambia mtu kitu , ingawa unauhakika kumng'ong'a kungefikisha ujumbe!
SI unajua maneno mengine jamii imeamua kuwa ni matusi?


Lakini....
... ukitukana sehemu sehemu fulani , kuna ambao wataamini wewe ni mtoto wa mjini.

Kuonekana mtoto wa mjini ni dawa ya kisaikolojia ya muda kwa mtoto wa mjini, kuhalalisha njia zozote za kufanikisha yale watoto wamjini wafikiriayo ni bomba na ni ujanja bila kuona aibu ingawa inaaibisha.

Ufundi wako wa kutumia neno kutukana, ni moja ya kipimo cha jinsi gani unakumbuka maneno uliyojifunza ukubwani.

Kama wewe ni kubwa zima kama mimi na unakumbuka matusi, basi akili yako inafanya kazi vizuri kukumbuka hata jinsi ya neno liwezalo kutumika kuomba msamaha au hata kuhakikisha lugha yako si chafu kama yangu katika uwasilishaji wako wa ujumbe .


Najua kama wewe unatoka Afrika ya mashariki na lugha yako ni Kiyao , Kikwere au hata Kijita kama mimi, unajua kutukana kwa kingereza.......

......Lakini.....
... ushawahi kumtukana mtu kwa kumkonyeza?

Tokea enzi za mababu, lugha inabadilika, na huzaliwa maneno mapya karibu katika lugha zote duniani karibu kila siku.

Maneno na tafsiri ya maneno ni dalili ya jinsi ilivyokuwa vigumu kwa binadamu kutumia neno kufikisha ujumbe au kujaribu kufikisha kauli.

DUH!
Ningependa kutumia neno kufikisha ujumbe hapa leo!
Lakini mbona hata nikitumia neno sieleweki?

Ningependa kutumia neno kuelimisha hapa leo!
Lakini mbona walioelimika bado hubakia na kutokuelimika kwa kibinadamu kama hatuoni elimu yao kutatua siri ya nini muhimu kwa binadamu?

Swali:

  • Unakumbuka jinsi wanaojua au pia wanasiasa wetu ambao wengine tunawaita MUHESHIMIWA Raisi, watumiavyo neno kuwatusi wananchi kwa kuwaahidi neno ambalo hubakia kuwa ni neno tu bila vitendo?
  • Unakumbuka neno ulilotumia kudanganya kakitu ambako kamesababisha uwe na amani rohoni leo hii kutokana na watu kukaaamini kaneno na kuacha kufuatilia kwa vitendo unafanya nini?
  • Unakumbuka kuwa utamu wa neno, ni uwezo wake wakutumika kudanganya au kusema ukweli?
  • Uongo mwingine si huitwa fiksheni au porojo na huchukii ukisimuliwa?
DUH!

Naheshimu neno na maneno, lakini kumbuka vitendo inasemekana ndio huongea kwa sauti kubwa kama unataka kumpa mimba au kupewa mimba ambayo matunda yake , ndugu jamaa na maadui wataweza kupotezea muda kwa kunyoshea kidole.

Vitendo vingine hata ukiviona , unaweza kujifanya hujaona ili usitamke neno.

Hebu tumuangalie mbwa akifanya kitendo...(samahani kama utatafsiri kitendo cha mbwa huyu kwa neno matusi au PUNYETO!SAMAHANI lakini kwa FIKIRA zako POTOFU au NZURI!)

DUH!

Siku hizi inasemekana wajanja hutumia neno hata kwenye nyimbo, neno ambalo mwingine ataita ni matusi na kudhalilisha mtu au watu hasa wa jinsia fulani.

SWALI:
  • Umestukia kila kizazi hutumia neno kusema kizazi kipya kimepotea kutokana na matumizi na tafsiri ya neno?
  • Umestukia ni miziki ya aina fulani tu ndio ina asilimia kubwa ya wasanii watumiao neno ambalo laweza kutafsiriwa kama tusi?
  • Kwanini?
NAACHA BASI!

NAWAZA TU USIKONDE!

AU?

Msikilize RAY J akikuimbia huuu wimbo ,(samahani ,hatumii lugha nzuri kwa watu fulani!Sishauri usikilize maneno katika wimbo kama wewe ukosensitivu na neno liwezalo kuwa tusi au wewe ni mtoto. Sikiliza kama kwa kawaida wewe si mfuatiliaji wa nyimbo zinasema nini.)...............

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP