Binadamu kwa madoido!We acha tu!
>> Friday, April 06, 2007
Napenda kukiri kuwa kuna watu wafanyavyo vitu vyao huwa hawanichoshi hata siku moja kuwa sikiliza au kuwaangalia. Lakini mara nyingi nashindwa kuacha kuzinguliwa na jinsi binadamu wanavyotengeneza vikorombezo mbalimbali vya aina mbalimbali kwa ajili tu ya kutaka kuwadaka binadamu wenzao kimawazo hata ki..... nakadhalika.
ukiangalia matambiko mbalimbali binadamu amfanyiayo Mungu wake hutaacha kuzinguka na madoido aonyeshayo. Wengine watalia huku wamenyosha mikono juu wengine watainama, wengine watalala juu ya misumari, ilimradi tu kumuonyesha Muumba au mauunguzaji jinsi gani wanamaanisha.
Duh!
Halafu hili swala la Mwenyezi Mungu watu wengi wanamuona kivyao!Halafu kila mmoja hakawi kuhisi mwenzie kapotea.Hapo ndio kasheshe.
Kinachoniacha hoi kingine ni jinsi binadamu akitaka kuonyesha madoido jinsi wachaguavyo mavazi yaendayo na madoido. Basi wengine watachagua kanzu, wengine vibwaya na vibuju , makofia makubwa kwa madogo na kadhalika kadhaa.
Ukweli ni kwamba hili swala la madoido nadhani mara nyingi tukubaliane tu halina mpango , lakini linaleta viutamu na vituko vyake ambavyo labda ni muhimu kwa sababu tumeamua tu kua ni muhimu .
Swali:
Hivi duniani binadamu anajali vitu muhimu?
Muhimu yako unaikumbuka?
Sasa....
Kwasababu tuko katika kipindi cha pasaka kwa wakrito na wakristu ngoja tuangali madoido katika kanisa la Holy Sepulchre
Hapa naona utaona jinsi madoido ya wanakanisa. Cha ajabu ni kwamba ingawa hapa ni miongoni mwa vipengele vya ardhi wakristo wavioanishavyo sana na yesu , huwa wanabwangana hapa kuhusu nani anamiliki kishkaji sehemu. Sasa hapo ndio madoido yanapo nishinda . Maana mpaka watu wanabwangana katika sehemu waziitazo takatifu. Duh!
Lakini wengine wanaonyimwa kuonyeshwa madoido yao hapo wameamua kuhamia huku kwa Garden Tomb
Lakini achana na madoido ya dini zihusianishwazo na Mungu. Turudi katika uchawi.Wachawi kwa madoido huta waweza. Ila wachawi wakizungu huwa wananiacha hoi na madoido yao pia . Maana hawakawii kukuuzia DVD ujifunze nawe.
Swali:
Hivi kwanini wachawi wa Kiafrika wasirisiri sana?
Hebu wajifunze kwa hawa hapa chini.....
Sasa kama kunamchawi yeyote atakaye tufanyebiashara yakuuleta uchawi huu karne hii tuwasiliane basi:-)
Lakini ushastukia wajanja wengi haswa hawa wanadini , wanasiasa, waigizaji na nasikia hata wachawi, ni wabunifu sana wa matumizi ya sauti. Wanajua jinsi ya kukutisha, kukufanya uwaamini, na hata.......
Lakini wote mimi nawaamini kwa kuigiza.
Duh!Kabla sijaendelea ngoja nikuache na vuduMaana hii ya wadominika imeanza kuuzwa. Ya Benin na kwingineko sijasikia bado.
Sasa Tanzania vipi? Madoido ya nguvu za giza kuexport lini?Maana nasikia kuna wajanja wanatengeneza radi na kadhalika.Naamini zao la radi pekee linaweza kukomboa wengi hapa duniani kwa jinsi tesivyopendana,
Ee Bwana eeh !Kama msherehekeaji basi Pasaka njema!
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment