Maswala ya maandamano na kupandisha Mori
>> Thursday, April 19, 2007
Kudai haki ni haki ya kila mtu, hivyo naamini kuandamana katika kudai haki ni haki ya kila mtu.Kupandisha mori ni ubinadamu, hivyo sidhani kuwa ni jambo lakushangaza kuona wadau wamechachamaa.
Sanaa ya kupandisha mori, mkwala na kugombania swala nahisi linakaujuzi ambako watu hukapuuzia.Ukicheki taarifa za habari zinazogusia maswala ya waandamanaji hukawii kujionea jinsi wadau walivyofuzu katika sanaa ya kuwakilisha ujumbe. Hukawii kuona kundi likiimba , kuzomea au hata kutumia silaha ndogo ndogo kama mawe kuwalenga wababe wenye bunduki.
Kinachonidaka kinamna ni saikolojia ijifichayo nyuma ya mtupa jiwe.
Nachojiuliza ni, ni nini wanafikiria wabebao bunduki hasa pale wakubalianapo kihoja na madai ya waandamaji waliopo mbele yao.
Kinachonizingua ni jinsi nchi mbalimbali zikabilivyo waandamanaji.
Bongo hukawii kupigwa virungu au hata risasi ukiandamana na kukutana na askari walio tumwa kukutawanya.
Lakini kuna kitu kingine ambacho mara nyingi huwa nakiona kwa wadaio haki,ni swala la mori kuchanganyika na lugha ambayo unaweza kushangaa mara nyingi. Unaweza ukastukia wanaodai haki za kuleta amani wakawa wanaimba au kupayuka maneno yaashiriayo mauaji na hata yakiukayo maadili ya haki wadaiyo.
Hebu cheki maandamano ya katuni hapa.....
Nadhani hapo juu hukawii kuona jinsi gani mchoraji mmoja wa Tanzania awezavyo kugeuza watu wadaio amani kuamua kuwa Watanzania wote ni kitoweo halali.
Sasa...
Ndio najua maswala ya kurahisisha majibu ya swala ni rahisi kwa binadamu hasa kwa maneno.Hivyo nakiri kutojua sana nini huendelea ndani ya kichwa cha binadamu akiamua, sasa basi, liwalo naliwe!
Lakini vilevile utasemaje ukisikia kuwa Wamasai huwa wanaweza kukupa dawa ya kupandisha mori ukitaka kukasirika kisawasawa?
Lakini tukiacha utani kuna baadhi ya Mori wapandishazo watu mimi naona zinapitiliza.Eti utasikia kuwa katika maandamano yakupinga mashindano ya U-miss huko India baadhi ya waandamanaji wakajichoma moto!Duh!Yani kabisa mtu kajimwagia mafuta ya taa au petroli halafu kajitia kibiriti kupinga mashindano ya U-miss!
Lakini ndiyo hivyo tena hataki tamaduni zao zichafuliwe na haya matamaduni machafu.Sasa haya matamaduni machafu mara nyingine kuyapiga vita yanataka jicho lionalo kote. Je, televisheni haichangii zaidi kuharibu tamaduni ikiwamo pia swala la mitazamo ya uzuri na matendo ya watu?Sasa ukijichoma kupinga u-miss ukaacha kujichoma mbele ya kituo cha televisheni ......Du ngojea niache hili swala
Lakini hebu cheki wenzetu wa Northen Ireland wafanyavyo maswala.....
Hawa jamaa walifikia hadi kupiga mawe watoto wa chekechea kisa wamekosea njia. Haya maswala ya Orange Order
ya wa protestanti ukichanganya na ya wakatoliki basi huwa kasheshe.
Nachoshindwa kuelewa ni jinsi nchi mbalimbali ziwathaminivyo watu wake kitofauti.
Naamini pia jinsi serikali iwakabilivyo waandamanaji na wafungwa ni jinsi ionyeshavyo ithaminivyo utu wa watu wake.
Eti...
Mkimbizi Afrika msosi apewao ni tofauti kabisa na mkimbizi Kosovo.Wakosovo bajeti yake kubwa.Hapa labda tutasema kuwa ni kwasababu wao kwa wao wanapendeleana.
Sasa...
Muandamanaji Dar kirahisi anaweza kupigwa virungu au hata risasi na Mtanzania mwenzake hata kama anakimbia tayari. Halafu unaweza kusikia Ujerumani wamewatawanya waandamanaji kwa kutumia maji.
Duh!
Nakubali kila mtu anatumia uwezo alionao kushughulikia swala akabiliano nalo.
Swali:
Hivi lile swala la kumkabili mtoto kwa kumchapa Tanzania linanguvu sawa na lakumnyima kutazama TV pale sehemu sehemu?
Kabla sijaliacha swala la kukabiliana......
Kali ni ile niliyoikuta Scandinavia ambapo wafungwa huwa wanalikizo, halafu hukawii kukuta kuwa unafanyanaye kazi sehemu na ukonaye bar ila yeye ni mfungwa kwasababu anarudi jioni jela.Halafu eti anateseka na kuapa kuacha kale katabia kaliko mfunga.
Ushastukia lakini kuwa mara nyingi kumtesa binadamu ni rahisi kuliko watu wengi wafikirivyo na wafanyavyo?
Tukirudi kwenye maandamano hebu wacheki kidogo Wa-South Afrika hapa...
Halafu kama ulivyosikia, eti kundi hilo lililokuwa na mchanganyiko wa weusi na weupe lilikuwa linashiriki nyimbo za kuapa kuua weupe.Duh!
Swali la pembeni:
Ushawahi kupiga mkwala mtu wakati unajua akicharuka utakimbia?
Mimi nisikufiche nishawahi kufanya hivyo halafu nikachelewa kukimbia, basi wachanibwengwe!
Lakini tudai haki zetu!Lakini pia tukumbuke wakati tunadai tunasema nini na mara nyingine tujiulize kuwa hivi ni kweli hii haki ni yetu?Hebu mcheki fisi akistukia kuwa yuko na washkaji wakutosha amfanyiavyo Simba....
Usiwaonee huruma mara nyingi ni simba waporao fisi kitoweo.
Samahani usizinguke sana!Alhamisi njema!
Lakini tukumbuke mpandisha mori na mpandishiwa mara nyingi ni damu moja.. Au ngoja nimuachie Junior Reid
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment