Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukitaka kupigana!

>> Tuesday, April 24, 2007

Kwa kawaida ya binadamu huchagua kugombana na yule aaminiyo anamuweza kumpiga.
Ukiona njemba , mara nyingi ni rahisi kughairisha ugomvi.
Hii imetusababishi dunia ambayo njemba kunaanga anajinoma kweli.

Lakini.......
Baadhi hata kama sio manjemba, wakistukia mnyonge hawakawiii kumuonea.

Duh!
Lakini ushawahi kustukia mpaka watoto wadogo wengine wakikustukia mnyonge wanakuonea pia?

Inasikitisha wanyonge kwa wanyonge huchaguana wenyewe kwa wenyewe wakishindwa kukabili njemba mbabe.

Lakini......

Kama wewe ushawahikushuhudia mtoto mdogo akitaka kumzidi dada au kaka yake katika kudai haki yake kutoka kwa mama, anaweza kushinda si hata kwa kutumia mabavu asiyokuwa nayo, huwa anatumia ile silaha yake ya kulia. Akishalia basi unaanza kuona mama anaanza kufikiria labda mtoto apewe tu yale maziwa au ule mdoli.

Sasa....
Mtoto aliliapo kitu mara nyingi hupata haki yake.
Lakini jinsi anavyokua staili hiyo yakudai haki huishiwa nguvu.Toto kubwa likilia linaweza hata likapigwa konzi anga nyingine.

Najiuliza tu sisi nchi masikini ,tulio halalisha misaada ni haki yetu, staili yetu ya kuomba misaada kwa haki inakipingamizi kizingatiacho umri wa nchi?

Samahani!
Niko mawazoni tu....Usistuke sana.Haya tuendeleze.....!
Pata Steel Pulse

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 8:35 pm  

Simon!
Ulishawahi kuchonganishwa na mwenzako kwa kuchorewa mstari? Umenikumbusha utotoni tulikuwa tukifanya hivyo. Ukikanyaga we kidume na mwingine akiukanyaga naye kidume basi ndodi zinaanza. Ka u-myonge huwezi ukanyaga mstari.

Anyway, mawazo yako ni mazito. Binafsi nimechoshwa na huu wimbo wa kuombaomba misaada. Siyo siri Kitururu, kila kongamano linaloandaliwa kuhusu Africa ni kuelezea matatizo tu. Hivi ni hakuna lolote tunaloweza tatua bila kuomba?

Hoja ya umri imetulia maana hata mtoto ukifikisha miaka kadhaa wazazi wanajitoa kukusaidia.

Baadaye

Anonymous 8:40 pm  

Umenikumbusha Mugabe.... ukimpiga...wamuonea..ukimwacha wamwogopa.

Simon Kitururu 8:44 pm  

@Mtanzania: Mara ya mwisho kuchorewa msitari nakumbuka vizuri.Ilikuwa songea nikiwa shule ya Msingi Mfaranyaki. Halafu nilipigwa raundi ya kwanza.Nikadai tuvue viatu.Nikapigwa tena nikadai kanitilia pilipili machoni.Haafu kajamaa kwa umbo kalikua kadogo kwangu:-)Sikutaka raundi nyingine tena mpaka tukahama Songea.Hivyo unaweza pia ku under estimate uwezo wa mtu.Huyo jamaa mpaka leo namkumbuka jina.Alikuwa naitwa Deo.Sijui tu jina la Mzazi wake ningeweza kumtafuta.

Kuhusu hayo mengine najiuliza sana hata mimi....

Simon Kitururu 8:49 pm  

@Serina:Kweli tupu ulichosema.Asante kwa kunitembelea!

Jaduong Metty 6:22 pm  

Simon,
Aisee hii ya umri wa nchi na kuwa ombaomba...imenikuna. Nadhani naweza kui"expandi" kidogo kwenye ka-ukurasa kangu..kama utaniruhusu.

Simon Kitururu 7:55 am  

@Metty:Endeleza tu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP