Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ushawahi kutungiwa jina halafu likashika?

>> Friday, April 06, 2007


Kuna watu wakikikutungia jina au hata wakitunga neno linashika. Kuna wengine hata wajaribu nini jina halishiki na wala kale kaneno watakako kukafanya maarufu watu wanakaacha kushoto.

Katika baadhi ya watu jina lao kama halishiki kama lilivyo basi watu hawachezi mbali na jina lake.Tukianzia na Amerigo Vespucci. Huyu jamaa kutokana na vyanzo vya habari vingi tu, ndio inasemekana aligundua Marekani na sio Christopher Columbus kama isemekanavyo.
Inasemekana misafara ya kadhaa Mzee Chris alikuwa anaishia katika visiwa kadhaa kama West Indies nakadhalika. Lakini haya yote inategemea na vyanzo vya habari tofauti kuegemea sehemu tofauti.
Tukirudi kwa Amerigo, huyu ndio inasemekana alichangia sana uchorwaji wa ramani ya marekani. Kwa kushirikiana na mchora ramani waenzi hizo maarufu aitwaye Martin Waldseemüller
Huyu mchora ramani alipomaliza kuchora ramani ya dunia bara la Marekani akaliita America kwa kuhusisha bara hilo na stori za Amerigo na mtazamo wa Amerigo aliompa.
Katika historia utakuta kunakipindi wachora ramani walitaka kubadili jina hilo kutokana na mashabiki wa Christopher Columbus kumpiga vita Amerigo kuwa muongo. Lakini wapi jina likan'gan'gania mpaka leo. Sitaki kuingia ndani katika swala hili la Christopher Columbus na Amerigo nani mkweli au muongo. Lakini nafikiri wote tutakubali kuwa wadau wa Christopher Columbus wamefanikiwa kumuekajina lake masikioni mwetu kuliko wadau wa Amerigo. Kuhusu kwanini likaitwa america na sio amerigo, kuna stori nyingi. Lakini iliyo shika ni kwamba mabara yote yalikuwa yanachukuliwa katika majina ya Kike. Africa, Europe....nk yote ni majina ya kike enzi hizo.
Lakini....

Lakini poa tu ukimuita mtoto wako wakiume Africa. Sikuizi yote zembwela , ngoma ya ukae.

Afrika , hili jina kasheshe. Wengine wanadai hawa jamaa waitwao Afri kutoka Tunisia, kuwa wamechangia.
Wengine wanadai limetokana na neno Aprica la kilatini nimaanishalo sehemu yenye jua.
Wengine wamedai kuwa linatokana na neno la kigiriki Aphrike limaanishalo bila baridi.

Lakini unajuatena hakuna haja hapa yakuingia sana. Nachotakakusema kuna kamjamaafulani sina uhakika nani lakini nahisi ni kajamaa ka bara jingi kakasema na jina liwe Afrika. Na likawa.

Lakini....

  • Ziwa Victoria tumeenda mbele sendema kurudi nyuma sendema. Lakini pamoja na kujua jina lake la kweli, Watanzani wengi bado twaliita Victoria.
  • Dar-es-Salamu-Duh !Hivi Mzizima lilikuwa naubaya gani?
  • Na kadhalika kadhaa. Najua unajua majina kadhaa tuyatumiayo au
Usitishike.Labda jina ni jina tu. Au?
Mimi mwenyewe nimefanikiwa kuitwa majina mengi. Nayameshika.Lakini chaajabu vikundi tofauti vyaniita jina tofauti. Hakuna noma lakini.
Nimejaribu kutungia watu majina na yameshika. Lakini nawaonea wivu walio tungia mpaka barazima jina na lika shika.

Duh!Kumbe wivu mbaya eeh?
Lakini si kweli kuwa kila wivu ni mbaya. Ukifanya vitu poa nivihusuduvyo sitakuloga napata nguvu tu ya kujaribu zaidi.

Sasa Baadaye basi!
Ngoja nikuache na Sina Makosa na Soukous Stars

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP