Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Generali Idd Amini Dada akiongea, duh!

>> Wednesday, April 04, 2007

Kama ukipata muda angalia hii kitu. Mimi sisemi....

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 5:49 am  

Huyu Idi Amini ananikumbusha aina fulani ya maafande. kwa mtazamo wangu alikuwa sio mwerevu sana kwenye filamu hii. Kama alivyoeleza mipango yake ya kuvamia uyahudi halafu akamuonyesha mpiga filamu drili ya uvamizi laivu... sijawahi kusikia jenerali wa jeshi akionyesha taktiki kabla ya vita kupigwa.

Halafu kigezo chake cha urafiki na mtu ni tafrija tu. Ati Moshe dayan alikuwa rafiki yake kwa sababu alimfanyia tafrija - siku chache baadaye akavamia entebe!

Alikuwa si mwanasiasa - hasa pale alipotaka kutuma posa amuoe Nyerere. Mwanasiasa gani asiye na diplomasia...

Kiburudisho safi, sijaona The Last king of Scotland - lakini hii orijino kiboko.

halafu Blogi yako imekuwa bomba sana kwa mtindo huu mpya.

mwandani 5:49 am  

Huyu Idi Amini ananikumbusha aina fulani ya maafande. kwa mtazamo wangu alikuwa sio mwerevu sana kwenye filamu hii. Kama alivyoeleza mipango yake ya kuvamia uyahudi halafu akamuonyesha mpiga filamu drili ya uvamizi laivu... sijawahi kusikia jenerali wa jeshi akionyesha taktiki kabla ya vita kupigwa.

Halafu kigezo chake cha urafiki na mtu ni tafrija tu. Ati Moshe dayan alikuwa rafiki yake kwa sababu alimfanyia tafrija - siku chache baadaye akavamia entebe!

Alikuwa si mwanasiasa - hasa pale alipotaka kutuma posa amuoe Nyerere. Mwanasiasa gani asiye na diplomasia...

Kiburudisho safi, sijaona The Last king of Scotland - lakini hii orijino kiboko.

halafu Blogi yako imekuwa bomba sana kwa mtindo huu mpya.

Simon Kitururu 12:06 pm  

@Mwandani: Huyu jamaa katika filamu hii na hata katika The last king of Scotland alikuwa kichekesho. Lakini huu ni mtazamo tu. Nimesoma baadhi ya maoni kwa Michuzi, kuna watu wamemsifia kuwa anafaa kuigwa. Eti ni bomba la mwanasiasa.Jamaa nachomsifu alikuwa anajiamini kwelikweli.Chochote kimpitiacho kichwani alikuwa anaamini ndio ukweli.Nafikiri moja ya kazi ngumu hapa duniani ingekuwa ni kuwa mshauri wa Idi Amini.

mwandani 6:46 am  

nadhani katika filamu hii pia alisema anaamini ndoto zake za usingizini. Akiota tu anafanya!

Anonymous 6:55 pm  

Ingawa simuoni kama kiongozi wa kuigwa, Idd Amin Dada namvulia kofia. Huyu ni bwana ambaye kusoma na kuandika kulimpa tabu. Ila aliweza kutumia mbinu mbalimbali kuwahadaa Waingereza na baadaye Obote hadi akaja kuwa rais. Alikuwa na ndoto, akaifanyia kazi, akawa rais wa nchi akiwa hajui kiingereza au kiswahili sawasawa. Akiwa ni mbumbumbu. Kumbe umbumbu wa darasani sio kikwazo kwako kutimiza ndoto uliyonayo.

Waandishi waliowahi kumhoji wanasema kuwa maswali mengi makali waliyokuwa wamepanga kumuuliza au shutuma walizokuwa wamepanga kumpa zinatokomea wanapokaa naye chumba kimoja kumhoji. Wanasema alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukufanya umwamini na kumhoji kirafiki.

Kuna mambo mengi alikuwa akifanya unajiuliza mbinu hizi alijifunzia wapi? Wakati viongozi wengi husoma vitabu na kuwa na washauri waliomaliza madarasa yote ili kupata mbinu za kutawala, Amin alikuwa akianzisha mbinu hizo mwenyewe bila kujifunza toka vitabuni.

Alikuwa na mbinu moja ya ajabu na kinyama aliyoitumia kwa watu aliokuwa ameamua wauawe. Kama mtu huyo ana jina au nafasi kubwa nchini, basi Amin alikuwa anaweza kumkaribisha ikulu ale chakula cha jioni na kunywa mvinyo. Wanapiga picha ambazo zinatolewa magazetini zikimuonyesha Amin na huyo mtu wakicheka kwa furaha na urafiki wa hali ya juu. Kisha baada ya siku tatu, idadi ya siku tunazoambiwa yesu alikufa, unasikia huyu jamaa katoweka. Baadaye unasikia amepatikana akiwa ameuawa baada ya kuteswa.

Urais katika mfumo wa kisiasa kama wa Uganda enzi za Amin sio kazi rahisi. Kuongoza nchi ya kidemokrasia ni kazi rahisi sana. Ila kuongoza nchi ya kidikteta, kujenga utamaduni wa ukimya na woga kwa wananchi wote, kuchunguza nani maadui zao na kuwaondoa duniani...aliwezaje kunyamazisha nchi nzima? Hofu. Alijua kuwa silaha kubwa kabisa dhidi ya mwanadamu ni hofu. Alijua binadamu wanapenda sana uhai. Binadamu wanaongopa, mara nyingi, jambo lolote ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao. Amin alijua ukweli huu na akautimia ipasavyo.

Tuache hayo, hivi kuna mtu mwenye uhakika kuhusu Amin kuivamia Tanzania? Je ni kweli aliivamia Tanzania kisha sisi tukajibu au habari ya uvamizi huu ilizushwa kama propaganda ya kuhalalisha vita vya kumtoa madarakani kutokana na kuonekana kuwa tishio la usalama Afrika Mashariki?

Anonymous 3:54 am  

[color=#000000]
Как жизнь? И кстати.. есть мега мысль по[url=http://www.pi7.ru] видео[/url] порталу Думаю вам понравится

[url=http://www.pi7.ru]вагина крупным планом[/url]
aнекдот для разнообразия :)

Вернулся керстьянин в глухую деревню из Столицы. Собралось всё село.
Сиддят, выпивают потихоньку.
Путешественник рассакзывает:
- Бвл в аком магзине инетресном "Секс-шоп" называется! Ну и магазжин, скажу я вам!.. Деевки насдувные продаются!
Тут самая бойкая на деревне тётка и спрашивает:
- А мужики надувные есть?
Мужик:
- Скажу четсно, - мужиков не вдел. Может, не ззаквезли? Но запчастей к ним - жо е#ен...

Я 7 часов блуждала по сети, пока ен вышела на ваш форум! Думаю, я дзесь осстанусь надолго!
пошу прощения за опечатки.... очень маленпькая клавиатура у PDA!

[/color]

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP