Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NAHISI KUNA KAKICHAA KIDOOOOOGO!

>> Friday, April 13, 2007

Pale....

  • Binadamu waendapo kupigana vita huku wakidai ni kwaajili ya kutunza na kuendeleza amani
-eti hata vita ya Iraki ni ya kuleta amani Asia katikati.
  • Wamagharibi watembeapo nusu uchi wakati wa kiangazi, lakini kuacheka waishio sehemu zenye kiangazi siku zote kwa kutembea nusu uchi
  • Waafrika waendapo makanisani zaidi ya hata wale wamagharibi waliowaletea Ukristo
  • Wairaki wapiganapo wao kwa wao kisa nani Mshia nani Msunni ,badala ya kumgombania Mmarekani na wenzake ambao wanawashutumu kwa kuvamia nchi.
  • Tukubalianapo uzuri U machoni mwa mtazamaji lakini hatuachi kuwaambia watu nani mzuri na nani mbaya.
-Kama uzuri umachoni , vipofu wanastukiaje maswala?
  • Miziki iitwayo ya asili- Afrika izidipo kupigwa kwa vyombo vya kizungu.
  • Mwanamume ajengapo uhusiano na matiti mpaka karibia kumshinda mtoto
  • Mwanamume ajengapo uhusiano wa macho yake na matako ya mwanamke
  • Katika dunia ya sayansi na tekinolojia zirahisishazo kazi kukuta wanawake wenye uhusiano wakaribu na misuli mikubwa ya wanamume.
  • Wanamume kwenye dunia ya sasa, ya sayansi na tekinolojia, waaminipo kuwa wanawake hawawezi kitu kwakuwa hawana nguvu za misuli kama wanamume.
  • .......................................nakadhalika kadhaaa mbili
Au?
Duh!Sijui kwanini Barry White yuko kichwani bado.
Ngoja basi nimuache na kibao Can't Get Enough Of Your Love Babe

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP