Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTAIFA mtamu , lakini ukizidi.........

>> Thursday, April 12, 2007


Bendera twazipepea sana! Nchi zetu twajivunia!

Hiki kitu Utaifa mara nyingi huchukuliwa kuwa ni kizuri. Na sipingi uzuri wake. Nachojiuliza ni , ni nini nafasi ya Utaifa wa mataifa yetu ya Afrika ambayo bado yanasumbuliwa na Ukabila, Udini nk au kifupi yanautaifa unaoendelea kujengwa?
Napenda kusema hivi kwa sababu mimi binafsi naamini kuwa Utaifa wa nchi kama Tanzania haujakamilika. Bado utasikia kuna Uzanzibar na Utanzania bara. Bado utasikia maswala kibao ya ukabila yakiwa msitari wa mbele.Ni kweli wakati wa kushangilia michezo tunapeperusha bendera zetu.Na siku hizi tumeongeza kuvaa bendera zetu ingawa bado nafikiri tunavaa zaidi bendera ya Marekani na Uingereza zaidi.

Tukiachana na hilo......

Utaifa ni hali mojawapo yakujibagua. Hii ni kusema mimi si wewe.Mara nyingi hasa ni kusema mimi ni zaidi ya wewe. Hii mimi si wewe inatumiwa sana hata na vikundi vya UNAZI na UNEONAZI katika kubagua waaminiwao kuwa si Wataifa wa taifa husika.Utaifa huu uliwanyemelea na kutaka kuwatenga hata akina Nyerere, Generali Ulimwengu nk.

Lakini....

  • Wakati tunadhamiria kuunganisha Afrika, je, tuachane na kung'ang'ania Utaifa?
  • Je, tung'ang'aniapo Utaifa tuuuche ukabila uondoke kabisa?
  • Je, katika ulimwengu huu wa utandawazi udaiwao kuwa dunia imekuwa kijiji, umuhimu wa Utaifa unamaana ilele?

SIJUI!
lakini....
Inasemekana mapinduzi ya viwanda tutayaruka Afrika na kuingia huku chobisi. Je , hii inamaana si lazima tupitiengazi zote za Utaifa kabla ya kuunganisha bara la Afrika.

Sijui!

Lakini nachojua ni kwamba chochote kikizidi huzaa madhara yake.
Wewe unafikiriaje swala hili?
Alhamisi njema!
Mpate Gil Scott Heron

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP