Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

GHAFLA!- Na kwa ghafla unaweza kubanwa hata na haja ISIYO kubwa kwa WENGINE!

>> Thursday, May 31, 2012

Ila GHAFLA,....
.... labda wala sio GHAFLA,....
...... kwa kuwa yasemekana kila kitu hapa DUNIANI huchukuwa MUDA,...
.... na inategemea tu na uharaka wa KIPIMO cha MTU kuhusiana na KITU uwezeshao  kugeuza SEKUNDE igeuke MWAKA.

Swali:
  • Si ghafla tu KIJANA anaweza kujikuta MZEE na anahangaika UZEENI kisa hakustukia UGHAFLA wa UZEE ukaribiavyo- kitu kilicho chelewesha KUJIANDAA?

Ndio,...
....labda inategemea tu na jinsi ulipavyo SWALA umakini,...
.... na kama humakini,...
.... kila kitu chaweza kuwa MITOKO YAKE  ni ya kighafla tu,...
.... na hapa wala siongelei  MTOKO kishahawa , kibaruti orgazimu ,ughafla wa KUHARIBU URAFIKI, Ughafla wa KUJIMIMINIA dhambi,ughafla wa kuingia ofisini na  KUJIFUNZA UFISADI , ufuska kiduchu wa GHAFLA mtu akihisi haonwi......
... au tu HATA  jinsi gani ghafla  UTAKAVYOSAHAU hii topiki,...
..... baada ya KUNISOMA!:-(

Swali:
  • Kwani si umeshawahi kubanwa hata na HAJA ghafla halafu baada ya kujisitiri ghafla UKASAHAU  ulivyobanwa kabla ya FARAGHA?

Ndio,...
.....labda kitu ``GHAFLA´´,...
...... hutegemea tu na spidi yako katika SWALA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia SIKU NJEMA!

Hebu Billy Ocean aingilie kati,...
... na kuongelea jinsi PENZI lilivyo leta maana GHAFLA katika kitu-SUDDENLY

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:17 pm  

Siku njema kwako Kadoda ..NA PIA AHSANTE:-)

Fadhy Mtanga 12:46 pm  

GHAFLA!- nikajikuta nasema duuuuh.!

Yasinta Ngonyani 1:06 pm  

EEEhh! Mtani Fadhy, nami GHFLA nimejikuta nasema duh! mtani kumbe upo:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP