Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA urafiki wa MWANAUME na MWANAMKE-labda UMPENDAYE mkwepe ili abakie kuwa ``JUST a FRIEND!!

>> Sunday, May 20, 2012
Kuna wadaio,....
.....URAFIKI usiowakinafiki kati ya MWANAUME na MWANAMKE,...
.... huwezekana tu kama RAFIKIYO hakuvutiii.:-(

Swali:
  • Si umestukia nimerahisisha hoja?
  • Na kwani si ni UNAFIKI kama kuna ajenda za siri katika udaiwao kuwa ni URAFIKI wakati kwako LENGO  ni zaidi ya u ``JUST a friend´´?

Ndio,...
..... labda udhaniaye ni RAFIKI TU,...
.... . uhusiano wenu umejengwa KINAFIKI kwa kuwa hakuambii tu kuwa atakacho ni zaidi ya URAFIKI tu wakuchekeana na kusikilizishana UDAKU!:-(

Wadeku hawa....

Ni uchokozi tu huu MKUU!
Nakutakia siku NJEMA!

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:33 pm  

Mimi naamini na najua unaweza kuwa rafiki na kijana/mwanamume...ila nasikitika sana nimempoteza rafiki yangu mpenzi. Nimeshangaa hapo kuwa wanawake wote wamekubali kuwa inawezekana lakini wanaume wanasema haiwezekani. Siku njema nawe pia mtakatifu Kadoda!!

Simon Kitururu 6:03 pm  

Ila nimekutana na watu kibao wafikiriao kama hao kwenye kideo. Mimi sina noma na urafiki wa jinsia tofauti!.... na pole kwa kupoteza rafiki Dada Yasinta!Siku njema kwako pia !

Yasinta Ngonyani 6:36 pm  

Simon! Ahsante sana ingawa maumivu ni makubwa...hata mie asilimie kubwa marafiki zangu ni wakaka!!!

sam mbogo 8:54 pm  

Utafiti mzuri sana mtakatifu.mi naamini ndiyo unaweza kuwa na rafiki wakike na wala msingonishane.Lakini inategemea urafiki wenu mliuanzaje nikitugani kiliwaunganisha,au kusababisha kuwa marafiki wa kawaida.lamuhimu hapa ni mazingira yaliyo sababisha muwe marafiki.pia katika urafiki huo inategemea mnakutana vipi mkiwa pekeyenu,au zaidi nawatuwengine,ili kuto towa mwanya wa kutamaniaana,je kama ni umbali nikiasigani,kama ni mipaka ni kiasi gani.namwisho,je ninani aliye anzisha urafiki huo,hili nalo ni muhimu.kaka s.

Simon Kitururu 8:59 pm  

@Kadala Yasinta: Kwa mara nyingine ``POLE sana kwa kupoteza Rafiki!´´ Pammoja san lakini...SI SIYE marafiki wengine bado tupo?

@Kaka S: Umemaliza yani kiaina!

Yasinta Ngonyani 12:16 pm  

Simon:-(

Simon Kitururu 12:20 pm  

Dada yangu mbona sikitiko?@Dada Yasinta

Yasinta Ngonyani 3:59 pm  

Sikitiko kwa vile huyo rafiki nilimpenda/nampenda sana na sasa hataki hata kuwasiliana nami:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 9:32 am  

da Yasinta?..pole kwa kupoteza rafikio...labda hujamtekenya kama mt. Simoni atekenyavyo juice ya ukwaju!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP