Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kweli YAKO , SIKU IKIANZA kukudanganya!

>> Wednesday, May 16, 2012

Katika MTU kuna ya LEO ,...
....na ya KESHO!

Na ya KWELI katika MTU leo ,...
..... labda mipaka yake ni tofauti na ya MTU huyohuyo  KESHO.


Swali:
  • SI KIBINADAMU kuna mpaka hata KUZEEKA?

Ndio,...
... labda UNOGEWAVYO na kitu leo ,...
..... ni tofauti na utakavyo nogewa na kitu KESHO.

Swali:
  • SI unakumbuka hata GLASI ya PILI ya PEPSI inautamu tofauti na GLASI ya kwanza ya PEPSI kama tu utamu wa BIA ya kwanza utofautianavyo na wa BIA ya TATU?


Ndio,...
.... kweli yako hata ya MKE wa KWANZA mwaka huu,...
.... inaweza kuwa ni UONGO kama itakuaminisha kuwa TAMU ni tamu tu kivilevile,...
... kitu kifanyacho ufikirie utamu wa MKE wa nne utakuwa ni uleule kama wa LEO wa mke wa kwanza.

Swali:
  • AU?
  • Kwani kwa mama watoto , mme anogavyo leo ndivyo atanoga kesho?


Ndio,...
.... hata tukiacha mengine,....
...... labda kumbuka MAISHA na LADHA zake sio MGANDO,....
........ na uking'ang'ania kuamini hata wali uleule ni MTAMU vilevile kisa unafikiri kwa kuwa ni uleule basi uko VILEVILE,...
......KWELI yako labda imeanza KUKUDANGANYA.


Swali:
  • Si yasemekana hakuna hata kitu kimoja hapa DUNIANI kibakiacho vilevile (tukiruka MUNGU) na kila sekunde  chochote kile ukikiweka kwenye bonge la darubini waweza kustukia MABADILIKO hata kama ni yale ya jicho lako au tu angalau jinsi UONAVYO?


Ndio,...
..... labda KWELI yako jana,....
.....LEO imeshaanza kuwa ``ONGO´´ ,...
.... na ukiibinua waweza stukia imeshaanza kukudanganya.


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu tuachane na hili na moja kwamoja tujiburudishe kwa ushambenga wa walionasiana....Au tulainishe tu zaidi kwa Zouk Love A l'ancienne

 

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:36 pm  

mmhhhh! kazi kwelikweli!!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP