Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAFIKIRI NI MARA NGAPI mtu aongeaye na wewe huwa ANAONGEA NA WEWE yakuhusuyo wewe na sio uliyompa nafasi tu KUYAONGEA ingawa alikuwa nayo kichwani kabla ya kukutana na WEWE?

>> Saturday, March 20, 2010

Kuna waongeleao WALI ukiwapa nafasi ya kuongelea WALI ,...
... wakati wakifikiriacho kabla ya wewe KUSAIDIA UWEZEKANO WA WALI KUONGELEWA  kilikuwa ni UGALI.:-(


Swali:

  • Unabisha?



Aongeacho mtu kuhusu WEWE kinawezekana hakikuhusu wewe na kinatokana tu na UZOEFU WA YASIYO KUHUSU YA AONGEAYE hasa ukizingatia hakuna amjuaye mtu mwingine vizuri UKIFIKIRIA  ingawa ni rahisi  hata kudhania kwa kuwa mtu ni ndugu yako basi kuna kitu anajua katika wako UBINADAMU.:-(



Swali:
  • Lakini wewe unajijua?
  • Unauhakika unawajua vizuri hata wazazi wako hasa ukifikiria hujui kwa uhakika walikutengeneza chumbani  au  migombani wakati wanatoka kwenye msiba wa jirani?
  • Lakini si unajua kwa kutojiamini na kujijua kwako kunaweza kuwa ndiko kusaidiako KUAMINI KWAKO kuwa labda kuna mtu mwingine zaidi yako ndiye anaye KUJUA zaidi?


Ndio,...
.... baadhi ya tafsiri ya MATATIZO MENGINE YA MTU hutokea kwa kuwa MTU HUYO MHESHIMIWA kajifunza na kufudhu kutegemea WATU WENGINE WANAFIKIRIA NINI KUHUSU YEYE mpaka wanafikia kuamini hata kitu kidogo ambacho wanakijua kwa kujiangalia kwenye KIOO kinategemea watu wengine waseme uzuri wa MIDOMO YAO KAMA BIRIKA ni mizuri namna gani au tu ni watu wazuri vipi kwa kuwa hawakosi kwenda msikitini.:-(


NIMEACHA!

Hebu tubadili kwa SANCHEZ kurudi ndude- FRENZY



Au Tanto Metro and Devonte warudie kitu-Gal say Wooee




Tanto Metro na Devonte warudie-Everyone Falls in Love

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP