Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UANDUNJE wa kujifunza kutoka katika matatizo WALIYOPITIA watu wengine!

>> Tuesday, March 23, 2010

Inasemekana ,...
...ni muhimu kujifunza  kutoka kwa waliofanya HICHO KITU kabla yako.:-(


Ndio inasemekana,...
....unaweza kutopoteza MUDA kwa  kuingilia BIASHARA ya chipsi mayai  kwenye eneo kama UTAJIFUNZA kwa waliotangulia kuuza CHIPSI MAYAI kwenye eneo na kujua kuwa  wateja hakuna na wapitao hapo huwa wana ulizia UGALI na sio CHIPSI MAYAI ambayo ndiyo biashara unaelekezea mtaji wako.:-(



Na inasemekana;...
....utatatua tatizo la KUTUNZA MUDA kwa kutegemea  kujifunza kutoka katika MATATIZO YA WENGINE na kuepuka kufanya matatizo kama ya hao wengine yawepia ni YAKO.

Swali:
  • SI umesikia kuwa INASEMEKANA kuna msaada UNAOTOSHA FUNDISHO kwa  kujifunza kuwa ukishika moto utaungua kutoka katika stori za wengine waliowahi kuungua kwa kushika moto kuliko weye mwenyewe kugusa moto ukaungua?





CHAKUKUMBUKA tu ni kwamba,...
....aliyetangulia kufanya  KITU anaweza kuwa alikuwa MFUPI  KULIKO WEWE na stori zake za ugumu wa kufikia KIDUDE unaweza ukawa uliongezewa ugumu kwa kuwa STORI YAKE KATIKA UGUMU ilijumlisha na KURUKIARUKIA KITU KUTOKANA NA UFUPI WAKE iliafikie KIDUDE kitu ambacho hakitakuathiri wewe ambaye NI MREFU VYAKUTOSHA na huhitaji kuhangaika  na mihitaji ya msaada wa kigoda ili kujiongezea kimo UFIKIE kidude.:-(



Swali:
  • Si unakumbuka WEWE sio YULE kwa hiyo ingawa ngoma ya SINDIMBA ni ileile yawezekana kukata kiuno KWAKO  ni rahisi zaidi kuliko YULE kwa kuwa wewe una kiuno kama NYIGU na ujazo wa MAKALI YAKO unatosha zaidi  NAKUIFANYA SHUGHULI YA  kuitingishia ngoma MAKALIO kwako kuwa rahisi zaidi kuliko  wengine wenye kiono kama kabati na makalio chapati ?


Ndio,....
.... kuna stori  za waliofanya UTAKACHO KUFANYA ambazo zaweza kukutisha kwa kuwa umeambiwa ni jinsi gani zilivyo washinda watu,....


.... lakini kumbuka labda walioshindwa SHUGHULI walishindwa kwa kuwa hawakuwa na kitu ulichonacho ambacho ni MTAJI WA PESA na wewe ukiingilia shughuli waliyoshindwa unachohitaji ZAIDI ni mtaji tofauti wa KUTUMIA AKILI ambao nao unao na SHUGHULI ZILIZOWASHINDA WENGINE ukiziingia kivyako mambo yatakuwa mswano.

Swali:

  • Hujastukia kujifunza kutoka kwa wengine NDIO MOJA YA SABABU  watu wengi huhofu kujaribu wenyewe hata wawiwezavyo?
  • Unauhakika hakuna CHA MANUFAA ujifunzacho kizuri kwa kuungua mwenyewe NA MOTO ili kujua maumivu ya MOTO badala ya kuogopa moto kwa kusikiliza stori za wengine za makali ya moto?

Kwa kifupi ,...
... labda kunakitu ulichojifunza kwa KUSIKILIZA STORI NA UZOEFU WA WENGINE,...
... ambazo ulihitaji kujaribu mwenyewe ili kujikwamua katika tatizo lakoLA SASA hata LILE la kuogopa KUTONGOZA MTU kwa kuwa anasifa za kunyima watu KUTOKANA NA STORI ZA WALIOJARIBU WENGINE ,....
....kwa kuwa labda KWA STAILI yako na kwa kuwa WEWE sio WALE ungekaribishwa katika ufalme na utukufu wa ukitakacho hasa ambao uko kwa UMUOGOPAYE kumtongoza.:-(


Kwa kifupi,...
....kwa kuwa CHIPSI MAYAI yasemekana haziuziki katika eneo yawezekana ni kwakuwa sio WEWE uziuzaye,...
... na ungeanzisha biashara ya CHIPSI mayai wewe na KWA UKARIMU WAKO ,usafi wa mgahawa wako, BONGE LA BATASAMU LAKO, na jinsi tu uwafanyavyo wateja wanajisikia wako nyumbani  , ungeweza kufanya mpaka  WAPENDA NGUNA aka UGALI  waanze kuja kula chipsi mayai mahali ambapo wengine wanadai hakuna wateja.:-(

Swali:
  • Umeshawahi kustukia KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WENGINE haina maana ndio ujaribu KUWAIGA HAO MTUZ WENGINE?


Ndio,....
.....kujifunza katika MATATIZO YALIYO WAKUTA WENGINE,....
... labda isiwe ni KUJITISHA TU kuwa  kwa kuwa wengine walipata matatizo basi na MTU MWINGINE atakutana na MATATIZO hasa ukizingatia labda wengine waliona NI TATIZO kwa kuwa ilibidi waonge mwili wakati KWA MWINGINE ASITAYE KWA KUTISHIKA NA STORI ZA WENGINE  tayari ni MALAYA kwa hiyo hilo la kuhonga mwili ili atatue tatizo la kupanda  cheo wala si TATIZO kwake.:-(

Ndio,...
... matatizo uyasikiayo YALIYOWAPATA  wengine ,...
...yana UANDUNJE  hasa kama HUYASTADI katika kunyambulisha yatakuathiri vipi hasa kwa kuwa WEWE sio WATU WENGINE na  staili na rasilimali zako za kuanzia AKILI mpaka ujiandaavyo tu kwa kuwa na kondomu  au tu polishi ya viatu kabla viatu havijachafuka yawezavyokutofautisha TATIZO LILELILE  kwako kutofautiana na hilohilo tatizo KWAKE.:-(


NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu twende Beira Msumbiji Djaaka wapoze mchecheto


Tubakie hapahapa Msumbiji Djaaka warudie ndude-Djogoro



Au tu James Brown na Lenny Kravitz wabadili tu tena kwa ndude-Papa's got a brand new bag

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP