Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Siku mtu akionjwa WAKATI kashadakwa na ugonjwa wa kichaa uitwao MAPENZI!

>> Saturday, March 20, 2010


Penda,....
..... na waweza kujikuta unashabikia vijulikanavyo na wanao kujua kuwa huwa vinakutia KINYAA.:-(

Penda,....
.....na waweza kujikuta aibu zinakuisha na kukusababisha uonekawaida na kudhani ni moja ya kuonyeshwa penzi kuombwa kitengeneza watoto sehemu ambazo zilitengwa katika majengo ili bila BUGUDHA watu wajifungie na KUNYA.


Penda,...
.....na waweza kujikuta kwa mara ya kwanza KWA SAUTI UNABISHANA na wazazi wako ambao busara zao ulikuwa unazitegemea kama ndio misingi ya maamuzi yako ya hata ni kwanini wewe INJINIA SIKU HIZI wakati ungekuwa MPISHI  MENYE FURAHA kama ungejisikiliza wewe mwenyewe kama ujisikilizavyo WEWE BINAFSI  NA KUWA NA UHAKIKA NA BUSARA ZAKO KATIKA MAAMUZI YAKO kama  hasa UJIAMINIVYO NA MAAMUZI YAKO katika kutiii ni muda gani ILIUSIJINYEE inabidi uende chooni KUNYA.:-(


Swali:

  • Unafikiri kama ungekuwa mtiifu kwa unaloliamini ni KWELI ,- kama ulivyokuwa MTIIFU KUHUSU YAKUHUSUYO WEWE BINAFSI kuwa iliusijikojolee ni muda gani inabidi uende kukojoa,... -unafikiri ni mangapi katika maisha yako yangefanana na wewe au picha yako ya dunia utakavyo iwe?
Ndio,...
... kuna uwezekano ukiongea na mgonjwa wa MAPENZI busara zako hazina maana kwa kuwa zinatetea kitu KWA KUTUMIA AKILI ZAIDI YA HISIA wakati uongeaye naye anatumia HISIA ZAIDI YA KUJADILI SWALA KIAKILI kitu ambacho labda ni aina ya UKICHAA.:-(


Na kwa bahati mbaya naweza kusema pia; `` NDIO´´,...
....UKICHAA uletwao na PENZI huweza kusababisha CHUNGU KIDOGO kuonekana tamu SANA  na kwa hilo labda MAPENZI ni aina tu ya UKICHAA.:-(

NIMEACHA!

Kumbuka NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na unaruhusiwa kulitukania!:-(

Hebu Ray Parker Jr abadili kwa kuwatetea wanaume katika ndude- I don't think MAN should sleep ALONE.
Au tu ASWAD warudie -Gotta find a wayAu tu ASWAD waendelee tu na ndude- I need UR LOVE

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 3:58 pm  

Duh! hii kamanyola na mawazoni ya falsafa ndani ya neo lenye mgodi wa dhahabu ya Geita kama tu vumbi la Mbinga... halafu ukiacha hilo vumbi tulia jumlisha na Tanzanite kisha mkuu niambie uhakika wa kizuri kuonekana kizuri kuwaku macho yanaangaza halafu kalumekenge pale gizani anakupiga chabo kwa kejeli.

ha ha ha ha ndiyo wazo la mkuu kama bakuli ya almasi ya kichwa cha nyerere na Gandhi jumlisha na shule ya vidudu ya Mfaranyaki sawasawa na raha za ksumiamshia hamu ya kujua mtakatifu ameandika nini?

SWALI nitaachaje kujifikirisha hapa? Niende wapi kupata mgogi wa UjingaBusara kama siyo kwa mtakatifu wa wapare?

Simon Kitururu 5:22 pm  

@Markus: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP