Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UBINADAMU DHAIFU uletavyo mapungufu mpaka katika kile KITU watu HUNUNUA!:-(

>> Tuesday, March 16, 2010

[Tahadhari: Taralila hii KUNAUWEZEKANO  ina wazo lililopinda!:-(]




BINADAMU katika anunuayo:....


....katika CHAKULA,...
....LABDA katika MAPUNGUFU hununua msosi akifikiria UTAMU badala ya VIRUTUBISHO VYA MWILI ambavyo kwa BINADMU ndivyo muhimu kiafya na UZIMA.:-(


Katika WACHUMBA ,....
.... labda hununua hata kwa mizawadi LIMTU ZIMA na MITABIA YAKE MIBOVU wakati labda wahitajicho katika mtu ni SEHEMU ZAKE TU BAADHI au tu zile za siri , - kitu kisababisha BINADAMU huendelea  kujikuta CHUMBANI  yuko na Limtu LIZIMA.:-(


Katika fulani  DINI,....
....kwa sadaka na MWENENDO labda MTUZ hujinunulia STAILI YA MAISHA  kama IHESHIMIWAVYO NA BINADAMU badala ya kustukia havinunuliki VIKUZA IMANI vile vilainishavyo woga wa  MUNGU MWEMA lakini ACHOMAYE VIUMBE alivyoviumba KATIKA wabadaye UZIMA.:-(


Swali:
  • Unafikiri KIBINADAMU ni rahisi kununua samaki bila shombo yake?
  • Kwa BINADAMU unafikiri kuna anunuacho ambacho hakina makapi hasa ukifikiria hata katika chakula kitamu KILIWACHO ni asilimia ngapi huja na kile ambacho BAADAYE binadamu hukiita  mavi?


Ndio,...
....LABDA katika UDHAIFU WA KIBINADAMU huwezi kununua SAMAKI bila MIBA yake.:-(


Na NDIO,...
....labda kila BINADAMU anunuacho lazima kiwe KIKUBWA zaidi ya ahitajicho na akinunua GARI basi amenunua na matatizo  YA GARI LAKE  na akinunua CHAKULA kitamu basi HICHO  lazima kije  na uzito utakaogeuka mavi yake. .:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
...labda katika kila kitu anunuacho BINADAMU ni KIKUBWA kuliko MAHITAJI YAKE,....
....na labda hata chupi inunuliwayo NA KIGOLI imezidi UKUBWA kama inaziba tako zima KAMA nia ya asili ya UTUMISHI WA CHUPI ili kuwa ni ili izibe matundu mawili tu YA SIRI ya KIGOLI yaliyo mbele na  SEHEMUSEHEMU ZILE  fulani katika ramani YA  YALE  makalio YAKE.:-(

Swali:

  • AU?

Ndio ,....
...labda hata uendeayo SHULE ili ujisikie UMEELIMIKA yamezidi UKUBWA kuliko MAHITAJI YAKO ndio kisa  katika MIA ya uyasomayo darasani  labda ni moja KATIKA HAYO  ambalo UKIKAA VIBAYA  utakiona cha mtema kuni  kikweli  MAISHANI NA KUKIKUMBUKA  UKIJUTIA kwa kuwa DARASANI hukuelewa hicho MAANA YAKE .:-(



.

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !:-(


Au tu tumpate Ex Plantashun mwingine a.k.a 2FACE IDIBIA akija na Wyclef Jean katika ndude- Proud to be AFRICAN



Au tubaki tu hapahapa Nigeria Ex Plantashun Boiz  2FACE IDIBIA aje na R.Kelly waweke twist katika wimbo wa ya MAD COBRA katika -FLEX


Au tu MAD COBRA mwenyewe arudie classic -FLEX

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 2:40 pm  

Mkuu hii kwangu ni post ya mwaka, kama ni award, basi hapa nimekupa.
Watu wengi hununua ladha tu, na wala sio vilivyomo ndani yake. Yanapotokea yasiyotazamiwa kwa upeo tulio ingia nao kichwa kichwa tunaanza kulaumu, laiti kama tungejua kuwa nanunua yai hili laweza kuwa safi au viza, tukilikuta viza tutasema nilijua yakhe, lakini kama umelipa nafasi ya uzima tu, ukilikuta linatoa shombo ya nguvu unatema mpaka utumbo wako.
Ila mkuu suala la kula halafu chakula kikatoka kama... :-)

Yasinta Ngonyani 5:55 pm  

Katika WACHUMBA ,....

nanukuu".... labda hununua hata kwa mizawadi LIMTU ZIMA na MITABIA YAKE MIBOVU wakati labda wahitajicho katika mtu ni SEHEMU ZAKE TU BAADHI au tu zile za siri , - kitu kisababisha BINADAMU huendelea kujikuta CHUMBANI yuko na Limtu LIZIMA.:-(" mwisho wa kunukuu. hapa pamenipendeza!!

PASSION4FASHION.TZ 10:28 pm  

Lol...mtakatifu Simon hii blog yako huwa inanifurahisha sana,huwa siwezi kutoka hapa bila kutabasamu,hiki nacho nikipaji mungu kakupa,hongera sana.

Simon Kitururu 2:48 am  

@Mkuu CHIB: Asante kwa kuipenda hii
@Da Yasinta: :-(
@Passion: Asante Dada yangu!:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP