Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BABA n'takusemelea kwa MAMA! OooooHO!

>> Wednesday, March 17, 2010

[Tahadhari: Wazo linatapatapa katika TARALILA HII!]


NIA ya kumsemelea MTU kwa mtu,....
..... inaweza kutoa SIRI ya MTU WA TATU  ASEMELEAYE MTU ya anawafikiriaje hao watu wawili ajitahidio kuwaunganisha kwa MSEMELEO.:-(


Kuna wadaio PIA kuwa ukisemelea mtu,...
.... nia yako ni kutaka tu UKWELI ujulikane na  SIO KINGINE,...
...na ikitokea kama unayemsemelea AKIPATA KIBANO basi hiyo huwa ni BONASI  tu kama kwenye CHIPSI dume ilivyo KACHUMBARI ,....

....NA NI BONASI tu PIA  kama  UTAPATA FARAJA SANA TU  hasa ikitokea ukashuhudia matunda yale YAKUSEMELEA KWAKO - yale  ya KUGOMBEZWA kwa MTU, kubinywa KWAKE makende, KUFINYWA au tu KUDHALILIKA kukifanikishwa kutokana na wako MSEMELEO.



ILA kwa bahati mbaya ukiangalia tabia za watu,...
.... utastukia KWA KAWAIDA afikiriwaye ni MNYONGE ndio HUSEMELEWA kwa MBABE ili ikiwezekana ishuhudiwe akigawiwa MKONG'OTO au angalau KUGOMBEZWA kidogo baada ya MSEMELEO.:-(

Swali:
  • Unafikiri KIINI cha KUWASHWA kwa mtu mpaka ASEMELEE KITU kwa MTU huwa ni kweli ni NIA UKWELI UWE WAZI  watu tumjue anyaye pembeni ya choo na KUFUTIA UTAJIRI kwenye ukuta wa choo ni nani au nia ni KUJIFAJIRI kwa MSEMELEAJI kwa KITENDO CHA KUSEMELEA?
  • Unakumbuka mara ya mwisho uliposemelea MTU?

  • Unafikiri kwa kawaida Tanzania , BABA akisemelewa kwa MAMA ina -nguvu?


NABADILI kidogo;....

Ndio,....
..... kunauwezekano hata ukiisemelea SERIKALI YA TANZANIA  kwa WANANCHI,...
..... wananchi hushindwa kufanya kitu  ingawa ndio wenye NGUVU na matokeo yake wengi twashuhudia  WASEMELEAO  WANANCHI kwa SERIKALI  kwa kuwa wanajua  SERIKALI ina polisi  na MAGEREZA-  bila kusahau vyombo vya habari ivitawalavyo ambavyo vyaweza kustua watu NCHI NZIMA  wasiona HATA NA mpango na WEWE  kuwa umekaa uchi bila kificha nyeti  UDHALILIKE kwenye jamii na kwa ALIYEKUSEMELEA.


NARUDI PALEPALE;.....


Ingawa kirahisi katika JAMII ya KITANZANIA inaweza kuaminika ``MAMA ntakusemelea kwa BABA´´ inanguvu zaidi ya ``BABA ntakusemelea kwa MAMA´´,...
.... ukweli wenyewe waweza kuwa  uko kinyume kwa kuwa labda MAMA ndio mwenye nafasi nzuri ya kumuadhibu BABA kama  adhabu aamuayo kuitumia NI ITUMIAYO AKILI ZAIDI na sio ile ioanishwayo na MIGUVU ya MISULI na PESA za BABA.:-(


Swali:

  • Si unakumbuka achangiaye kuonekana MWANAMKE ni dhaifu inawezekana ni MIMI na WEWE hasa weye mwenyewe MWANAMKE?

  • SI imekuwa kawaida kwa MWANANCHI kusemelewa kwa vyombo vya mabavu vya SERIKALI mpaka inasahauliwa ni WANANCHI HAOHAO WAOGOPAO SERIKALI  ndio bila wao hakuna SERIKALI hata hiyo isiyowajali yaweza kujitutumua kwa MAGUVU?

  • Unauhakika lakini BABA mwenye MIGUVU na MAMA wakianzisha vita baada ya wewe kumsemelea BABA kwa MAMA hawezi kudedi MDINGI ambaye kazoea kupikiwa na MAMA MWENYA AKILI  na kutarajia MINOFU YOTE MIKUBWAMIKUBWA ya BATA apewa yeye kwenye ZE MLO ambao watoto huambulia mchuzi na  mabakimabaki ya chembechembe za mnofu wa BATA kabla BABA hajarudi usiku KALEWA?
Ndio,...
NIA ya kumsemelea MTU,....
..... inaweza ikawa ni kujisikia vizuri tu kwa ASEMELEAYE hasa kama anachokisemelea hakimuhusu ASEMELEAYE kuwa UNANANILIHIII   ambacho   hata KISIPONANILIWA hata afanyeje HATA KINANILII  YEYE .:-(

Ndio,....
.... sibishi kuna ASEMELEAYE mtu,....
.... kwa nia ya kusawazisha kosa ili UNAYENANILII usijezoea tabia MBAYA ambayo itasababisha UNANILIWE hapo baadaye.:-(


NIMEACHA wazo MHESHIMIWA na kumbuka hili ni wazo tu ambalo ni  RUKSA kutolielewa!:-(
BWANA na BIBI wasifiwe!


Tupoze basi kwa kumsikiliza tena Mheshimiwa IDD AMIN




Tuendelee kidogo na Mheshimiwa Idd AMIN


Na tumsikilize kidogo tena Mheshimiwa  KIBAKI



Sasa twende kwenye KIPELE nikilengacho bila utani-Where Will We Find Tomorrow's Leaders?

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP