Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA unakumbuka BUSARA YA ulichofundishwa SHULE YA VIDUDU!:-(

>> Friday, March 12, 2010



Labda ,...
...SHULE ya kuishi na WATU KATIKA MAISHA ulishaIMALIZA kwa ULIYOJIFUNZA shule  ya VIDUDU a.k.a CHEKECHEA.:-(



Swali:

  • Unakumbuka CHEKECHEA wanafundishwa nini hata kama wewe hukuenda hizo shule ziitwazo za VIDUDU?

TWAWEZA KUJIKUMBUSHA lakini kuwa busara za chekechea  hazina maringo katika KUTEKENYA UMUHIMU kwa kuwa  ukiwa chekechea UTAFUNZWA yaleyale ya muhimu  sana MAISHANI kama:

  • KABLA ya kula OSHA mikono
  • UKIMALIZA kula osha MIKONO
  • KABLA ya kuvuka barabara angalia pande zote uhakikishe hakuna gari


  • KABLA ya kunya vua chupi na usinye pembeni ya choo
  • UKIMALIZA kunya chamba na osha mikono


  • USIMFINYE mwenzio

  • KUJAMBA mbele za wenzio ni tabia MBAYA

  • USIMUIBIE penseli, peremende AU KARANGA mwenzio


  • KAMA unaumwa sema
  • Waheshimu BABA na MAMA

  • Na kama.....NA kadhalika kadhaa za nk...



SWALI

  • Umeanza kukumbuka MAFUNDISHO hayo?
  • Unafikiri ukifuata hayo tu uwezi kula BINGO maishani hasa ukikumbuka digirii zako huruka somo la USIMFINYE MWENZIO?



NAACHA!
Lakini ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(





Lakini LABDA endelea nami KUSIKILIZA HAWA ambao wasemacho  kama umefundwa  weye  utaendelea tu kuwa MHESHIMIWA hata wakati uwasikilizao ni  DAS EFX kama tu enzi zile za ndude -ALRIGHT


AU Fu-Schnickens waendelee tu na wajanja wajuao hizi ndude wakiri kama wanajua nani ni - True Fuschnick



AU tu MAD LION abadili kidogo lakini AACHIE mchezo uleule katika  -REAL TING

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP