KUWAZA!
>> Tuesday, March 30, 2010
Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,....
...ningewazia chakula na kuruka kufikiria mpaka kama NI KWELI hakuna mavi yenye ulemavu .
Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,..........ningechagua kuwaza ya busara na kukwepa kuwaza kuwa moja ya alichonacho MWEREVU ni upumbavu.
Ningechaguliwa cha kuwaza,....
.....labda NI KWELI ningekuwa muda wote ni mpumbavu.
Lakini KWA kuwaza upumbavu,....
.....kuna astukiaye WEREVU wa watu JINSI ulivyotokana na upumbavu.
Na napenda neno ``PUMBAVU´´,....
..... kwa kusababishia KUNIIKUMBUSHA kustukia wale werevu.
NA ni wewe MWENYE busara na werevu ,....
....hasa kwa kuwa tu WEWE na sio MIMI katika yangu ya kipumbavu.
Swali:
- Ushawahi kustukia kuwa upumbavu unavyowasaidia wengine hasa kama kwa werevu wako imesababisha unashindwa kufanya kitu kipumbavu?
- Mpumbavu afanyaye kitu na MWEREVU ajizuiaye kufanya kitu unafikiri ni nani mchango wake UTASTUKIWA zaidi na jamii?
- Unafikiri MPUMBAVU kwa kawaida anajistukia?
Hebu The Roots wabadili zaidi kwa ndude- Proceed
Au tu The Roots warudie kitu - The Seed
Au tu A Tribe called quest watulize kwa - Oh my god
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment