Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tufikirie tu UTAMU wa wimbo mzuri wenye MANENO MABAYA!

>> Wednesday, March 24, 2010

Utamu wa wimbo una mambo yake,...
... ndio maana ukichunguza utakuta MPAKA kuna mtu anapenda wimbo FULANI  kwa kisa tu unaneno TAKO.:-(


Na avutiwavyo mtu na wimbo kila mtu staili yake,....
....na kuna wadaio WIMBO MZURI sio mirindimo wala maneno na ni jinsi uwakumbushavyo KITU au MTU na hata wakikuimbia huo wimbo hawafikirii maneno yanasema NINI na yana MAANA GANI na haiwaingii akilini labda huo wimbo ni matusi KWAKO.:-(


Swali:

  • Kwani kwako  wataka kusema wimbo mzuri  ni ule uuelewao maneno yake tu?

Ndio,...
... kuna ambao uzuri wa wimbo ni VIDEO yake.


Swali zaidi kidogo:
  • Huwa unafikiria LAKINI  ni kwanini unaupenda wimbo fulani?
  • SI unajua ni  kawaida  maeneo fulani  kusikia nyimbo za KANISANI kwenye baa na kuna wajipozao baada ya kuzini kwa kusikiliza nyimbo mpya za dini?


Ndio,...
.... labda unavyosikiliza wimbo  unachosikia ni VIPENGELE  VYA MAISHA katika MAISHA YAKO VIGUSANISHWAVYO na wimbo  na wala huusikilizi  wimbo kama idhaniwavyo kwa MIRINDIMO YAKE na MANENO YAKE   kitu ambacho chaweza kuwa KIMESHASABABISHA umewahi  kuukatikia kiuno wimbo wa msibani badala ya kuufanya ukusaidie kutoa BONGE LA mchozi.:-(


NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA!

Hebu JOE ARROYO alete - YAMULEMAO


Hebu na Tshala Muana alete pia ndude-Sikila

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 11:15 am  

Kuna watu hupenda wimbo sio kwa ajili ya maneno, bali kwa midundo yake.
Fikiria mtu hajui hata chembe ya kispaniola, lakini unamkuta ni mpenzi mkubwa wa nyimbo za salsa, Iglesias nk, na anajaribu kuziimba, lakini ukimuuliza maana ya wimbo anaweza kuku..... tu.. la nguoni.
Upenzi wa wimbo unategemea hisia za masikio ya mtu, na wala sio maana ya wimbo

EDNA 1:19 pm  

Kuna nyimbo na nyimbo, mfano Reggae na nyimbo za dini huwa nataka tu kuelewa kinachoongelewa ndani ya huo wimbo haijarishi ni mdundo wa aina gani.Nyimbo nyingine huwa nazingatia mdundo, sauti ujumbe sio sana.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP