Ingawa ni MKOJO wako LABDA kunasababu unachagua CHAKUKIKOJOLEA!
>> Sunday, March 07, 2010
Kila kitu na mahali pake,....
..... na katika eneno KIUTU hata mavi huchaguliwa mahali pake.
Na kirahisi waweza kusahau kuwa KANISA SAFI lenye WAUMINI WASAFI moja ya siri ya WAKE USAFI ni lilihitaji choo pia KISICHO NA UHUSIANO NA DINI kisaidiacho walopendeza na KUNUKIA VIZURI waendelee kunukia vizuri NDANI YA KANISA kwa kuwa KINYESI CHAO kina mahali pake,...
Na kirahisi waweza kusahau kizuri kama DINI ndicho kikukumbushacho UNA DHAMBI na kukata makali ya utamu wa DHAMBI na katika USIKILIZIAVYO TAMU na kugeuza janja ya kidude ni ujinga kwenye UJINGA mahali pake,.....
Kabla sijasitisha WAZO hili banangenge,....
Swali:
- Si unakumbuka SHILINGI ina pande mbili wakati unaitumia kununulia KIDUDE kimoja?
- Na si unakumbuka MAVI katika HISTORIA YAKE AMBAYO SIO NYINGINE yaliwahi kuwa CHAKULA kitamu?
Ndio,....
.... LABDA,.....
..... kuna sababu MKOJO wako mwenyewe unauchagulia JIWE na sio kitanda chako katika FARAJA YAKO ya kuukojoa.:-(
Na yawezekana mpaka HASIRA ZAKO labda ukifikiria VIZURI utastukia huwa kuna WATU UWACHAGUAO wakuwatolea MIKIKI YA HASIRA hasa kwa kuwa kama tu ulivyochagua KUTOLIA CHAKULA CHOONI kuna ambao UMEWACHAGUA waendelee kuamini wewe kwa kuwa PADRI basi INALIPA UKIENDELEA kutoonyesha zako hasira KWA kujulikana MPOLE ingawa wote twajua kama ni BINADAMU wahitaji dozi kadhaa za kukasirika na UNA HASIRA ULIZOZICHAGULIA MAHALI PAKE kwa kuwa kuna wageni ,...
.....kama huna kilema.:-(
Swali:
- AU?
- Unafikiri kama una dhambi hakuna sehemu ulioichagua ambayo kirahisi unajisikia huru ZAIDI kurudia DHAMBI?
NI WAZO TU HILI MKUU na ni ruksa KULIBISHIA huku umetoa macho!
Hebu Sean Paul + Rihanna warudie- Break it OFF
Au tu Sean Paul na Blu Cantrell wabadili tu kwa -BREATH
Au tu Lady Saw na Beenie Man wabadili zaidi kwa -Healing
DAIMA nikipata muda huwa nipo na WADAU.....
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment