Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DOZI ndogondogo ZAKUMKUMBUSHA MWANAWANE wakati anaringia yake TAALUMA!:-(

>> Wednesday, March 10, 2010

Kuna wasahauo kuna WASUKUMA MKOKOTENI ambao,...

.... HAWAKUPATA tu  bahati kusomea URUBANI lakini akili za kupaisha ndege wanazo.

Na kuna VIGOLI ambao,...
... hawakujifunza tu TAALUMA YA  UCHAWI lakini  ukileta za kuleta  uwezo wakujifunza KULOGA wanazo.

Na kuna MASISTA na MAPADRI ambao,...
..... WITO umefanya wapunguze BAADHI ya matumizi ya utupu na kibonyezo  ambavyo   WALIOOA na... au tu MALAYA wanaweza KUBOBEA na KURINGIA katika tumizi fulani , LAKINI ikumbukwe nguvu ya tumizi la HIVYO VIDUDE  halafu wakatubu baadaye MASISTA na MAPADRE wasiooa AU kuolewa wanazo.:-(

Swali:
  • SI unajua KUJUA KITU na KUFANYA KITU vyote huhitaji  nafasi ya kujua na MAHALI  na muda wa kufanya kitu, KITU AMBACHO cha weza kufanya ambaye angekuwa INJINIA WA MELI  kawa fundi bomba?
  • SI unakumbuka  KUJUA kitu  ni nishai na MWANAFUNZI anaweza kumzidi MWALIMU katika kujua hicho kitu?
  • Unauhakika ni wewe mwenyewe ndio uwezaye kuelewa kitu  au  ni mazingira tu ndio yawezayo kukufanya WEWE ndio uwe mwenye taaluma ya kitu?

LAKINI,....
...labda ,...
... ni bahati tu  kuwa na TAALUMA ambayo wengine hawana ingawa labda kuna mwenye KICHWA ZAIDI cha hiyo taaluma  ambaye anaringiwa na mwenye TAALUMA.:-(


 Swali katokori:

  • Hivi inawezekana KURINGA kwa dozi ndogo ndogo ni AFYA ndio maana binadamu anakipaji hicho  au KURINGA ni kama tu nywelenywele NDEFU ZAKIKWAPA au zile za chini kidogo ya kitovu cha MKUBWA ambazo shughuli zake na umuhimu wake KUUJUA ni mpaka PROFESA fulani afanyie uchunguzi?


NI TAFAKURI tu HII MHESHIMIWA  ambayo waweza kujikumbusha wakati unamnyolishia mtu TAALUMA YAKO na  wala usikonde!
SI unapata MSHAHARA?

NIMEACHA!:-(

Hebu tubadili kwa kuhudhuria harusi na vifijo WAKATI mdada akichukua mdada jumlajumla



Au tu twende KENYA kukutana na CANNIBAL na SHARAMA waongelee-KICHWA KIBOVU



Au tu tubaki TZ JHIKOMAN arudie ndude-MAPENZI



Au tu twende ALGERIA Khaled Hadj Brahim a.k.a Cheb Khaled aendeleze kwa -AICHA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP