Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ilivyo sura ya MAJUNGU KABLA hujapigwa MAJUNGU yanayokorokochoa KUNAKO!

>> Thursday, March 11, 2010

 Vitu vingi KUHUSU WEWE  vinasemwa kila siku,....

..... na waweza kuvidharau kama  VISEMWAVYO kivitendo   havikuathiri na KISAIKOLOJIA uko ngangari kukabili ya watu maoni.

Na katika vinavyosemwa kila siku,....
..... vyaweza kuwa NI AMBAVYO UNAWEZA KUVIPUUZIA lakini yote hayo ni kwa kuwa ni VYA AINA zile zile ambazo UMEZOEA  kusikiaWAKWARE    WAKiPIGANIA mpaka kuchaniana  chupi na gwaguro na ndio siri  YAKO ya kujiandaa kuzoea na  KUVIPUUZIA na labda umeshashiriki pia KATIKA KUTATUA mishemishe hiyo ISIYOKUGUSA ya aina hiyo  kwa wahusika kuwapa VIDONGE VYAO  angalau kwa maoni.


Swali:
  • Lakini si inasemekana ni kweli KABLA hujalogwa UCHAWI ni porojo?
  • Na si inajulikana kila MTU ukimjulia huhitaji FIMBO kumpa adhabu?



Kila mtu ,....
.... ana kaudhaifu kake  na kuna MWENYE SURA MBAYA ambaye watu wamezoea kumtukania SURA kitu alichozoea NA KIRAHISI ANAKIPUUZIA ,....
....wakati  udhaifu wake uko kwenye MATEGE YA MIGUU ambayo bado hajazoea kutaniwa hasa kwa kuwa alikua NA KUKUZWA  afikiri anabonge la USAFIRI na hilo lilifanikiwa mpaka alivyopenda MTU na huyo mtu akamuacha akimwambia hawezi kuwa na kishtobe MWENYE  MATEGE  na mwendo kama MJUSI mjamzito.:-(


Kila mtu,....
...... ana kaudhaifu kake na kuna adhaniwaye ni  JASIRI KWA YOTE  na MAJUNGU  karibu yote yale ya kuwa yeye MWIZI , malaya, ANA kibiongo , NI JIRANI MBAYA kwa kuwa ni kweli  anajambaovyo  ananguvu  za kukabili na ANAYAPUUZIA,...

.... lakini  haki yanani akipigwa MAJUNGU yamuhusianishayo na kuwa yeye MCHAWI anakuwa kaguswa KIPELE cha UDHAIFU kwa kuwa hata yeye mwenye labda alihisi BABU YAKE alikuwa MCHAWI na maishani mpaka kilichomfanya  KAOKOKA au tu kuwa MSWAHILINA , yote ni katika kuhakikishia UMATI kuwa yeye ni BONGE LA MTU MZURI na  sio MCHAWI na kwa kumpiga MAJUNGU kuhusu uchawi kitu kihusianishwacho na kabila lake  ambalo KAMODIFAI JINA usilistukie kabila lake , KWAKE unakuwa kama UNAFANYA watu wageuke kwa KWAKO  kumpiga teke HADHARANI mjamzito.:-(

Swali:
  • Hujawahi kushuhudia jasiri wa kutania dini za wengine  siku akisikia dini yake inatukaniwa au AKISIKIA tu stori za kujambiwa kwa  kitabu  aaminicho ni kitakatifu katika DINI yake ?



Ndio,....

.....KABLA hujalogwa labda  stori za UCHAWI ni porojo,...

....NA kabla HUJABAGULIWA labda ubaguzi wa rangi ni porojo.:-(


Na kila mtu ana kaudhaifu kake,.......

....kama ni MWANAMKE usidanganyike ,...
....DUNIANI hakuna tako LAINI labda ndio maana MWANAMKE kwa MWANAMKE wakibwengana KATIKA KUTAFUTIANA MAUMIVU hushuhudii tako likilengwa kama vile NYWELE  ZIVUTWAVYO na kikubwa husikii ugomvi wa wanawake ukosao matusi na kelele za maneno kwa kuwa UDHAIFU wa mwanamke ili kuuchokonoa vizuri MAUMIVU wahitaji kutumia neno .

Swali:
  • AU?

Kila mtu ana kaudhaifu  kake,...
.... na kumbuka kwenye MWILI wa mwenye mijinguvu kama SIMBA ,...
kwa kawaida kama ni DUME lazima kuna maeneo yenye KORODANI au  MAKENDE  laini na yenye kusikilizia MAUMIVU VIZURI  tu hata kabla hujasema neno.:-(

Swali:
  • AU?


Na kama HUJAPIGWA majungu yakakuingia vizuri ,...
.... labda tu ZAMU yako bado na wakupigao MAJUNGU kuna kitu hawajui kuhusu WEYE.:-(


Na inaweza kuwa KIMAJUNGU KIMGUSACHO umjuaye kwa kuwa na mpenzi MWANANA WA JINSIA TOFAUTI  yaweza kuwa ni kigumu kukibuni kwa  kuwa HUAMINI  kwake KIUDHAIFU  BENDERA yake ni HUYO MPENZI MWANANA ALIYENAYE na ukweli  ni kuwa BAFUNI akioga anamichezo yakujichezea mwenyewe KUNAKO ili  KUTUNZA NGUVU za kutunzia siri yake kuwa anahusudu watu WA JINSIA YAKE,....
......na kamwe hastuki kwa yale majungu yaliyo MTAANI WATU WALIYO YAVALIA NJUGA  kuwa eti yeye FISADI  na anapata MITOTO MIZURI  zaidi MTAANI  kwakuwa anahonga hela za SHIRIKA.:-(

Kwa kifupi,...
...MAJUNGU kuna yanayowasaidia kitu ambacho WAPIGA MAJUNGU hawajastukia.:-(


Samahani NAACHA !
Ila kumbuka HILI ni wazo tu  MHESHIMIWA!:-(



Hebu Touré KUNDA arudishe USTAARABU hapa kijiweni  DUH!

Aje kwanza na kitu-WAAR



Au tu Touré KUNDA amalizie na ndude-Wadini



Au tujifunze tu KUWA  misosi ipo

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP