Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI unaongea na MLEVI na unafikiri kunauwezekano ni POMBE inaongea!:-(

>> Sunday, March 07, 2010


KAMA wewe ni MSIKILIZAJI,...
... kunauwezekano umeshamsikiliza MTU na kustukia kalewa DINI.:-(


Na tatizo hujitokeza tu kama weye  MSIKILIZAJI,....

.... kwa kustukia kama  huamini YESU kuna MSOMI utakaye kujua mawazo yake LAKINI hoja zake zote zisizo na uhusiano na DINI zinahitaji  NUKUU za MWOKOZI YESU alisema nini  katika mtongozo wa hoja hata za UMASIKINI wa  MAMA NTILIE  kimwana ASHURA  wa karibu na soko la  bwimbwi lenye MBILIMBI na halihitaji BUSARA  zitokazo katika vitabu   vya DINI.:-(


Swali:

  • Unauhakika umewahi kuongea na MTU ambaye hajalewa KITU?
  • Unauhakika aongeaye ni wewe ikiwa uongeacho chahitaji unukuu BUDDHA alisemaje ili tuelewe stori zako za kungarisha UTU UZURI za hitaji midabwada?


ILA kwa bahati NZURI,...
....wakati unaongea na MLEVI unaweza pia kupata JIBU LA TATIZO LAKO la jinsi ya KUBINYA JIPU kama weye ni MSIKILIZAJI,...

..... kwa kuwa pamoja na uongeaye naye kwako kufikiri KALEWA anaweza pia akawa NDIYE MWENYE JIBU zuri zaidi lihusianalo na JIPU hasa kwakuwa aweza akawa yeye ndiye MTAALAMU WA MAJIPU.

Swali:
  • Si unakumbuka kama hujui kupika MAANDAZI unaweza usiwe unajua siri ya SHAVU NYORORO LA ANDAZI  ingawa HUJALEWA na si unajua kuwa MLEVI  anaweza akawa ndiye ajuaye VITUMBUA vinapikwaje?
  • Wakati unalalamikia walevi UNAUHAKIKA wasiolewa umewasikiliza kwa asilimia kubwa HUWA wanaongea nini?

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu LL COOL J abadili kwa KUPINDISHA aina za KIBUSARA kwa  kitu-I'm That Type Of Guy




LL Cool J aendelee kwa ndude - Hush




Au tu LL Cool J amalizie na AMERIE kwa ndude- Paradise

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP