Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

kWA bahati mbaya MUDA hauponyi MAUMIVU!:-(

>> Thursday, March 18, 2010

Ndio,...
....kunauwezekano UFANYACHO NDANI YA MUDA baada ya kuonja UTAMU ndicho KIKUPONESHACHO kumbukumbu ZA jinsi  ulivyowahi kuusikilizia UTAMU.:-(

Ndio,...
....kuna wasemao kwa ung'eng'e ``TIME HEALS´´ a.k.a ``MUDA UNAPONYA´´ ingawa mimi ningependa kukualika ukae mkao wa kufikiria uwezekano wa kuwa - ``IT IS WHAT YOU DO within that TIME  that DOES THE TRICK´´ a.k.a  kwa lugha ya wajanja-``NI UFANYACHO baada ya KUUMIZWA au KUSIKILIZISHWA UTAMU ndicho kinaweza kukusahaulisha na KUPONYA uyakumbukavyo MAUMIVU  au  tu ule wa lawalawa UTAMU´´.:-(




Swali:


  • Kwani ni kweli  ulifikiria maumivu na WIVU wa mwenye MPENZI aliyestukia MPENZI wake aliyekuwa anafikiri ni wake peke yake tu  anagawia na wengine UJANJA huwa yanaponeshwa na MUDA TU bila kwa hilo lijamaa aka HILO lililostukia linadokolewa penzi na wajanja kujishughulisha na kitulizo kingine ambacho labda ni KWA kujisomea KORANI na kumsikiliza mchungaji wa PENTEKOSTE?

  • Unafikiri ni MUDA TU na sio na michango ya vitu hovyo kama vile WALI , mikate na VIAZI  ambao vitakusaidia kusahau UTAMU wa UGALI NA MAHARAGE   hapo baadaye ukiamua kujisahaulisha tamu yake kwa kuwa inakukumbusha sana MBWA wako mpenzi alipozirahi na kufariki dunia?



Ndio,...
... labda MUDA haukuponyeshi  UKUMBUKAVYO utamu wa MAKANDE YALIYO CHACHA kama ndani ya muda baada ya kula PURE a.k.a MAKANDE yaliyochacha hautashughulika na kitakacho KURUDISHIA kumbukumbu ya UTAMU HALISI wa yale matamu MAKANDE.:-(



Ndio,...
....ukifikiria LABDA utastukia  ni KWELI kuna kitu umefanya katika muda  na sio MUDA TU ndicho kilichofanya hukumbuki vizuri ulivyotishika na DHAMBI baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kuifanya MAKUSUDI ndio sababu LABDA siku hizi unarudia HIYO dhambi makusudi KIRAHISI bila kujisikia vibaya sana.:-(


Ndio,...
....MATUMIZI ya MUDA na labda WALA sio muda ndicho kisababishacho kuna aina ya UTAMU huisahau na kunaaina ya MAUMIVU labda unailenga makusudi ili kujikumbusha jambo FULANI ingawa bila kufikiria ndio maana kuna MPENZI husahau maringo yake.:-(



NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na haki ya nani tena NIMELIACHA!

Hebu tubadili kwa kwenda kiduchu  BRAZIL  Sergio Mendes atuletee tena kitu-Magalenha




Au tu Sergio Mendes na The Black Eyed Peas warudie ndude-Mas Que Nada


Basi bwana , tubaki tu na Black eyed Peas ya enzi ZILE katika kitu kitukumbushacho wikiendi bado haijafika kiitwacho-Weekends

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:29 am  

Ninanukuu "Kwani ni kweli ulifikiria maumivu na WIVU wa mwenye MPENZI aliyestukia MPENZI wake aliyekuwa anafikiri ni wake peke yake tu anagawia na wengine UJANJA huwa yanaponeshwa na MUDA TU bila kwa hilo lijamaa aka HILO lililostukia linadokolewa penzi na wajanja kujishughulisha na kitulizo kingine ambacho labda ni KWA kujisomea KORANI na kumsikiliza mchungaji wa PENTEKOSTE?" Kwa mtazamo wangu naona hapa kuna uitilafu wa mahusiano na pia kutoaminiana ni afadhali kuongea nadhani kutapunguza maumivu na wivu pia. Duh! hapa kazi ipo tena kubwa tu. Upendo daima.

Simon Kitururu 5:24 pm  

@Da Yasinta: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP