Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA!

>> Wednesday, March 31, 2010

Waweza kustukia SIKU HIZI ,....

....Wanasiasa wanachukuliwa kama VICHEKESHO na WACHEKESHAJI wanachukuliwa siriasi!:-(

Kama unaona nachoona na KUSIKIA NACHO SIKIA siku hizi,....
...... unaweza kudhani MWISHO WA DUNIA umefika mpaka usome HISTORIA na kustukia dhambi nyingi zistukiwazo ZILISHA ANDIKWA KUWA ZINAFANYIKA tokea kabla ya  enzi za kina YESU na kuna waliodai dunia imefikia mwisho enzi hizohizo wakiwa tu vilevile siriasi.:-(

Swali:
  • Unafikiri akina FARAO wa MISRI nao hawakuwa na kitu wakiitacho SIKU HIZI?



Kuna uwezekano IDADI YA WATU imekuwa sana siku hizi,...
... na ukichanganya KITU HICHO na TEKINOLOJIA ZA HABARI zisababishavyo mpaka UDAKU KUPATIKANA kirahisi ,....
... labda kuna tunayoyasikia  TU zaidi SIKU HIZI ingawa yalikuwepo tu hapa DUNIANI toka enzi za madanga chee.:-(

Swali watu wenye imani fulani :
  • Unadhani baada ya ADAMU na EVA kufanya dhambi ya kula tunda , dhambi yao iliyofuata ilikuwa ni nini?
  • Ushawahi kusikia msemo hakuna jipa chini ya anga na kama KITU hakijafanywa na MTU basi kimefanywa na angalau mjusi?

Ndio,....
.... kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA,...

..... labda kibadilikacho hapa duniani ni staili tu  LAKINI MAMBO NI YALEYALE,...
....kama tu  salamu kubadilika  KUTOKA ``Mambo dukinaa! ´´ kwenda  ``Mambo POA!´´ na  salamu YA KISASA kuwezakwenda mpaka kuwa  ``Mambo Kukojolea dodoki!´´ - lakini zote zikimaanisha JIBU la  salamu HIYO HIYO ya tokea enzi ya kuwa ``Mwenzetu hujambo lakini!´´.:-(



Ndio,....
.... kama unasikia na kuona nachoona,...
..... labda HATA udaku  ni uleule kibadilishwacho ni MAHALI  lugha tu  itumikavyo  au itumikayo.:-(

Na haki ya nani  labda mambo ni kama SURUALI ,...
...iwe ni PEKOSI , kodrai  au hata JEANS ya nailoni lakini vyote ni suruali  na kupendeza  au kutishwa na jinsi suruali imbinyavyo tako mtu HUKO KUKO  tu machoni mwa mtazamaji na LABDA hakuna WATAZAMAJI wawili WAONAO na kuoanisha suruali na muonekano wa tako sawasawa.:-(


NI WAZO tu la GHAFLA MHESHIMIWA na wala usikonde kama unauwezo wa kula BAGIA !:-(


Namuachia SADIKI aendelee katika-Do You Hear What I Hear


Au tu Rick James abadili zaidi kwa ndude -Cold Blooded

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP