Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo tujikumbushe BIASHARA ya maiti UINGEREZA!

>> Thursday, April 01, 2010



DUNIANI kuna mengi ,...
....na hayo mengi kwa bahati MBAYA hutokea kona zote za DUNIA.

KWA Bahati mbaya MAMBO mengi ya AJABU kirahisi  husakiziwa WAAFRIKA au AFRIKA siku hizi  zidaiwazo zina mengi,...

.... lakini hali halisi  inaonyesha kuwa YA AJABU yako DUNIA NZIMA na cha ajabu kwako  chaweza kuwa ni kawaida mahali pengine SASA HIVI ingawa kuna kipindi LABDA yalikuwa ni kawaida HATA hapohapo ulipo katika upande huohuo wako wa  DUNIA.


Swali:
  • Unabisha?
Ukikuta STORI ya ajabu kutoka NCHI ZIITWAZO ZIMEENDELEA inakuwa kama  ni kitu cha ajabu  ,...
.....na chaajabu ZAIDI  ni kwamba  ni wale watokao NCHI ZIITWAZO HAZIJAENDELEA ndio wanakuwa wa kwanza KUSHANGAA na kuona ajabu kuwa   imekuwaje MFARANSA  mstaarabu ndiye anakula KONOKONO halafu ananiona miye wa ajabu kwa kuwa nagida KUMBIKUMBI na kwa kuwa  kwa mchoma mishikaki napenda kuagizia pumbu za mbuzi .[samahani katika  neno pumbu nilikuwa natakutumia neno LA KIHESHIMA ; ``makende´´:-(]

Stori kama ya juzijuzi ya JINSI YA KUMUANDAA PAKA MTAMU ya  mpishi maarufu wa KIITALIANO ilyosababisha sangambingo kwenye TV  katika kipindi cha La Prova del Cuoco  iliwakera WAITALIANO lakini katika wote nilioongea nao ,- watokeao KUNAKO BARA LA GIZA ndio nilishuhudia WAKITOA BONGE la mshangao zaidi  kuwa hawa jamaa wanavyopenda Paka na MBWA  kistaarabu sikutegemea kuwa walikuwa wanagida PAKA wala sio muda mrefu kwa kuwa bado kizazi cha wagida paka bado kipo- hasa kwa jinsi wajulikanavyo kwa kushangaa  wengine  wa pande nyingine za dunia wakati wanafaidi POPO wa kukaanga au tu  pale mitaa ya CHINA paka huyohuyo akibanikwa poa.:-(




OK!
Stori ya HISTORIA ya kula PAKA ITALI sio lengo muhimu la taralila hii ya leo ingawa KAMA UMEINGIWA MDADI WA STORI  ngojea niianzishie upya stori utamu ..

Basi  MUTU  MUKUBWA  ndani ya MAPISHI ITALY  kwa jina  Beppe Bigazzi alikasirisha WAITALIANO  kwa kutoa siri kuwa PAKA alikuwa KITOWEO MURUA TU  Italy. Watu walikasirika kwa kuwa wanaona hilo ni jambo ni shai kwa zaidi ya mtu kujamba makusudi mbele za WASTAARABU.:-(

AAAGH! endelea mwenyewe HAPA


...au pata tu  dondoo ya utamu wa NYAMA YA PAKA kwa maneno yake mwenyewe BEPPE BIGAZZI hasa kama umeshawahi kumdeku paka anakatiza halafu ukafikiria  kwa maringo yake inaweza kuwa KUMGIDA NI sumu.

 BEPPE anadai:
“I’ve eaten it myself and it’s a lot better than many other animals,” he told viewers. “Better than chicken, rabbit or pigeon.” He said that for optimum flavour the meat should be “soaked in spring water for three days” before being stewed.....


Ila kama nilivyosema LEO tujikumbushe BIASHARA ya MAITI UINGEREZA  katika enzi za ma-BODY SNATCHERS


STORI yenyewe ni   ...


Kuna kipindi  kufukua maiti na kuziuza Uingereza ilikuwa bonge la ujasiriamali ......

AAAAHG!  Hebu endelea mwenyewe HAPA na taralila ianzayo.....

``During the 17th and early 18th centuries, a grim profession emerged. A growing number of anatomists, keen to improve their medical knowledge, needed corpses on which to conduct dissections, which were often done in ‘theatres’, where members of the public could pay to watch............

Swali:
  • Si unakumbuka KUKUMBUKA idaiwapo AFRIKA hatuachi vita kuwa ULAYA  , Asia ,...na mpaka AMERICAS wana historia ndefu sana na ILIYOANDIKWA ya vita vya wao kwa wao ambayo imefanikiwa kuua vya kutosha tu labda hata zaidi ya AFRIKA ambayo hata jiografia yenyewe ilikuwa inafanya iwevigumu siye WAPARE kuwakong'ota vizuri WACHAGA mitaa ya Kilimanjaro?:-(

  • Kama unapenda kula nyama ovyo MTAANI unauhakika kweli hujawahi kula Kunguru wakuchoma? LIONE VILE!


NI MEACHA MKURUGENZI!
SIKU NJEMA!

Kumbuka...

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

o'Wambura Ng'wanambiti! 12:59 pm  

Katika ulimwengu huu wa kufakamia hata visivofakamiwa wawezajikuta umefakamia konokono ambaye kwa wengi wetu wataona kinyaaa!

Na je si wawezakuta hata vilivyomo katika hiyo chupa uipendayo katika tendo halisi la kugida si vilivopaswa kuwamo? Kuna wakati wanywaji wa bia hapa walikuwa wanashuhudia nywele ktk kinywaji na uchafu mwingine wa aina hiyo :-(

Nakumbuka pia wakati ule twasoma sekondari ambapo tulikuwa twabebwa na Treni kuanzia Mwanza mpaka Moshi via Dar ambapo tulikuwa tukiuziwa kuku wenye miguu mirefuuuuuu pale SARANDA!


Na pia tulikuwa tukiuziwa Maziwa yenye krim nyekunduuu. Baadaye njaambiwa na watani wangu kuwa ati yalikuwa madhiwa ya PUNDA...lol

Ni vizuri kujihadhari!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP