Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNACHOKISIKILIZA,... nani anakisema?

>> Sunday, April 04, 2010

[Tahadhari: Taralila hii inawazo lililokaa uchi!:-(]


ASEMAYE,...
...anaweza kuwa ASEMACHO ni kwa MTAZAMO wa waliomsemesha!:-(


Na kwa kuamini wakusemeshao unaweza mpaka kuamini wavuta bangi WOTE wamechanganyikiwa hata kabla huja kutana na mvuta bangi kama Barack Obama au Bob Marley na kusikiliza wakati wamevuta bangi wanaongea nini.:-(






Swali:
  • Si KUNA MWENYE UHAKIKA KWA KUSIKILIZA TU MTU KUWA mvuta bangi na asiyevuta bangi wanaguna tofauti wakati wanazini ingawa hajachunguza wasiovuta bangi wawili wanaweza wakawa wanagunia shughuli kitofauti   wakati wanafanya shughuli  KAMA WEWE ile ya mtindo kavukavu?
Na wamseshao mtu  AKASIKILIZA kwa bahati mbaya ni wengi,...
..... na kwa kusikiliza tu watu unaweza mpaka KUSTUKIA NA  kufikia hitimisho asemaye mtazamo wake ni kwamba NYAMA YA BATA NI TAMU ANAPATIA  kuliko ya KUKU hata kabla hujamshikilia kiuno njiwa  au hata huyo binamu ya KUKU ambaye ni  njiwa.:-(



Swali:
  • Si wewe kama MUISLAMU hustukia mapungufu ya aongeaye KATIKA KUATHIRIWA ki MTAZAMO  aongeacho  kirahisi kinatoa siri umsikilizaye walio muathiri ni wakristo na KIMUATHIRICHO HATA KATIKA KUFIKIRIA kwa kutumia akili kuwa kwa nini kuingiza na kuchomoa BANANGENGE  anakuita ni uzinzi  kwakua  fikira yake ya mzalisho imekaa KIKRISTO kama aliyemsikiliza kuwa MKE WA NNE  DHAMBI ?



  • WEWE kama MSABATO si unastukia staili ya asemaye YESU kama huyo ni MROMANI KATOLIKI hata kabla hajamgusia BIKIRA MARIA aliye BIKIRA ambaye  AMUITAYE BIKIRA Maria anakiri  alimzaa kwa kugunia mzao kama kawaida YESU?

NDIO,....
....labda UNACHOSIKIA labda jaribu kumjua ANAYESEMA NI NANI kwa  kuwa kama unasikiliza tu NAKUFUATA  bila kujua asemaye,...

...unaweza kuchanganyikiwa bila sababu HATA  ukinunua CHUPI isiyoruhusu KIPENGELE CHAKO KIPUMUE WAKATI KIMEBANWA NA KIFICHA NYETI  kwa kuwa umsikilizaye katika stori za chupi anaweza kuwa ni yule ambaye HAJAWAHI KUVAA chupi mpya.:-(

 Swali:
  • Unachosikia huwa unachunguza nani anasema hata asemaye  AKISEMA  hakuna ajenda ya siri  katika hilo ASEMALO hata kama limeegemea  kukufanya upende KAROTI ZAIDI  wakati wewe ni mpenda MAPERA?

NIMEACHA

Usikonde lakini  hasa kama weye ni miongoni mwa wamsikilizao POPE  BENEDIKITI katika maswala ya husuyo ladha ya  KONDOMU kuliko MALAYA  aliye wahi kupata mpaka gono wakati anacheza na kivalishwacho kondomu!:-(



Tupate KWA KUBADILI USTAARABU angalau  tukunyema kidogo ya UKIMWI kutoka kwa FRANCO akinyambulisha kiua nyege katika ndude-ATTENTION na SIDA


Au tu VYBZ KARTEL na SPICE walainishe swala tena kwa mkito - RAMPING SHOP






Nilikuepo kabla sijaondoka ULAYA kama

Photobucket

Photobucket


Photobucket


Photobucket

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 12:03 pm  

Haya mkuu, tumesoma ujumbe na maswali yako. Majibu hatuna
Nakutakia pasaka njema

Yasinta Ngonyani 12:51 pm  

Sawa! Pasaka njema Mtakatifu Simon:-)

Mzee wa Changamoto 1:16 pm  

Labda uwe topik ya WALIWAZA NINI kwani yawezekana kuwa uwazalo lina manufaa kama watu wataacha kuwaza watakavyo uwaze wewe na kisha kuwaza uwazazlo na namna iwezavyo kuwa msaada kwao.
Ile nadharia kuwa unasikiliza ilhali umeshaamua nani unaweza kumsikiliza hukwamisha mengi. Wapo ambao tayari wameshasema SAWA kabla hawajaambiwa kuna swali lihitajilo "sawa" hiyo na sababu kuu ni kwa kuwa kwa awasemeshaye, sawa ni sawa hata kama haiko sawa.
Unadhani wote wasiosoma hapa hawahitaji ELIMU hii KUJITAMBUA?
La hasha... Wanashindwa kujua uhitaji wa kujitambua na hivyo kuendelea kujipoteza katika harakati za kujitafuta.
Labda tubadilishiwe mfumo wa fikra ili asikiaye asikie kwanza kabla hajatambua anenaye.
Mmhhhhhh!!!!
Ni kama nami naanza kujipoteza katika kutafuta nimaanishacho
Naacha Mkuu
Nikutakie PASAKA kibonge yenye ubonge wa wema.
Blessings

Fita Lutonja 1:59 pm  

Kweli kabisa wavuta bangi siyo wote wanaakili panga hakuna kwa hiyo watu wasiwachulie hivyo kwani wapo wavuta bangi lkn akili zao kuzidi hata za rafiki yangu mgiri Socrete.

mumyhery 3:04 pm  

Simon kabinti kazuri mno mhu!!!!!!

Simon Kitururu 7:43 pm  

@Mkuu CHIB:Sijui kwanini nawasiwasi kuwa jibu unalo.:-( Ntajitahidi kukutafuta kama inawezekana ntumie namba yako ya simu uitumiayo kunong'oneza watu Bongo kwenye skitururu@gmail.com

@Dada Yasinta: Asatente lukuki! Nakutakia kila lakheri katika kuendeleza tamutamu ya siku za pasaka.

@@Papaa mubelwa: DUH umezidi kuniwazisha ni kiota kipara shauri zako! Asante pia kwa kunitakia heri kibonge!
@Mkuu FITA:Si utani ulichosema Mkuu!
@Mumyhery:
Ni kweli kimuonekano na kwa asali ya sauti na neno Kabinti ni katamu ila namsubiria DADA Yasinta amuache mume ili nimtongoze kwa hiyo ni bonge la tatizo.:-)

MARKUS MPANGALA 10:26 am  

katika kipengere cha Barak Obama na ndude ya jani ongeza na teja zuri zaidi ya bangi lakini ndude ile inamfanya sikilizwe saaaanaaaa eti anamiakili kuliko Nyerere asiyeonja ile ndude ya kufikiri tu jani la kisamvu hata bangi.

Utambuzi na kujitisha kuwa ile ndude ya bangi inaleta wehu kuwmbe wachungaji wanaozini au maksisi wa papa Benedkiti.

Na wale wanaowaibia Watanzania kila siku na kuwaletea maisha duni nao wanapata ile ndude sema niwaorodhesheee????

Umbeya tu mbona hwakamati ile ndude lakini mambo yao ni fyongoooooooo.

Yasinta Ngonyani 5:11 pm  

Wow:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP