Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati unafikiri UNAONGEA na MTU mmoja,.....

>> Wednesday, April 14, 2010

...ni vizuri kukumbuka UWEZEKANO uongeaye naye NAYA anaongea MUONGEACHO na mtu MWINGINE.



Na hicho ndio kitu kifanyacho KUWE NA UWEZEKANO siri umpayo mtu mmoja,....
....umewapa watu tisa na nusu  BILA wewe kujua.:-(



Swali:

  • Wakati unamtumia mtu mmoja text meseji umewahi kufikiria uwezekano  wa meseji hiyo ya siri kusomwa na kijiji kizima?

Ndio,....
... siri ya watu wawili na YA WATU MIA labda hazina tofauti  kinamna,.....
.... na ambacho sio wewe pekee ukijuacho KITU kuna uwezekano wote hicho kidude wanakijua.

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!

Siku Njema!


Hebu Mahotella Queens wabadili kwa - Jabulani Mabungu



Au tu Mahlathini arudie tu ndude-Kazet

11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:07 am  

Kumwamini binadamu ni jambo ambalo lataka moyo sana. Kuna watu ambao hawawezi kabisa kuwa na jambo ambalo wamelisikia peke yao ni lazima walisambaza na kuna watu ambao wanaweza kumweleza mtu kitu ambacho hakimuhusu kabisa. Ahsante kwa hili Simon:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! 11:35 am  

Ayaa! Mtakatifu, umenena. Sasa hata nahisi ile nilokutumia umeionesha pale kilabuni kwenye KOMONI...lol

o'Wambura Ng'wanambiti! 11:35 am  

Ayaa! Mtakatifu, umenena. Sasa hata nahisi ile nilokutumia umeionesha pale kilabuni kwenye KOMONI...lol

Koero Mkundi 2:17 pm  

DUH!!!!!!!!!!!!!!

chib 9:17 pm  

Yani Chacha umemwona mtakatifu ni mtu wa komoni :-)

o'Wambura Ng'wanambiti! 10:36 am  

@Chib: kwa kuwa wageni wangu wote hukutana nao ktk kilabu ya chibuku, komoni ama ze gongo manzeseeee kwa mfuga mbwa!

Ntaweza wapi viwanja vikubwa kama MALAIKA resort kule jirani na uwanja wa ndege Mwanza? :-(

Mzee wa Changamoto 12:11 pm  

Duh!!

John Mwaipopo 3:41 pm  

siri? siri ya mtu mmoja. siri ya watu wawili nadhani inategemea kudumu kwa uhusiano wa hao watu. baada ya hapo yaweza kuwa sio siri tena.

talk of sms? kitu hii imeleta vita ya dunia ya tatu katika mahusiano ya watu wengi tanzania. sijui huko mliko wengine.

Unknown 11:50 am  

Mmnh.....kifupi hakuna SIRI......!!

Bennet 10:06 pm  

Kweli siri ni ya mtu mmoja tu yaani wewe peke yako

malkiory 9:45 pm  

Kwahiyo, Kitururu tusemeje hapa, siri ni ya mtu mwenyewe? kama hakuna siri kati ya watu wawili au zaidi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP