Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwanini WACHEKAO WAKITEKENYWA kwa kawaida hawakuambii wana HAMU YA KUTEKENYWA !

>> Saturday, April 03, 2010

Kumbuka  tu,...
...KUCHEKA KWINGINE  kwa wakuchekeao KWAO ni SHUGHULI tu kama tu ile ya kubinya jipu  kwa kuwa tu jipu limeiva.:-(



Ndio,...
.. UWATEKENYAO wakacheka,...
..... WAJICHEKESHAO bila kutekenywa,....
....... wachekao kwa kuwa UMETEREZA na kuanguka kitu ambacho ni cha kusikitisha,...

... na wachekao kwa kuwa KUNA  chakuchekesha,....

... LABDA vicheko VYAO vyote hivyo  havina undugu  ingawa vyote vimefanya  mtu akenue meno.:-(




Swali:
  • Unauhakika kikuchekeshacho ni kichekesho?
  • Unafikiri ni kwanini mwenye huzuni kwa kawaida hatekenywi katika kutibu huzuni kama KUCHEKA ni furaha na kitekenyeo SEHEMU SEHEMU anacho?
  • Unafikiri UWALIZAO hawakuwa na hamu ya kutosha ya kulia ndio maana wamelia?
  • Kwa kawaida  WEWE UKICHEKA huwa inakuwa umechekeshwa au unajichekesha ?


Ndio,...
.... apendaye kucheka labda si kweli anapenda kutekenywa kama tu apendaye kula MAGIMBI labda hapendi umlishe MAGIMBI.:-(



NIMEACHA!
NI WAZO TU na kutolielewa RUKSA!

Ngojea tena katika kubadili hali ya hewa baada ya wazo lililokaa vibaya  Safari Sound Band watoneshe kidonda kwa ndude - Mama lea mtoto wangu



Santana aturudishe WOODSTOCK kwa mkito-Soul Sacrifice



Au tu na Jimmi Hendrix  ajaribu kupoza kwa KUKITA KIUTU UZIMA  kwa banangenge-All along the watch tower



Sijui kwanini lakini SANTANA ngojea tu adungishe pia na -Evil ways

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:30 pm  

Pasaka njema kaka Simon! nimeufurahia huo wimbo kukatika :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP