Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tamu ya KUJIDANGANYA,.....

>> Monday, March 15, 2010

.... inaweza KUSABABISHA kuwezesha kila  UNACHOJISIKIA UKISEMA kukigeuza ni KWELI.:-(



Swali:
  • Si unajua INASEMEKANA ukirudiarudia kudanganya WATU  KITU  unaweza kuanza kukiamini mwenyewe HICHO  KITU kuwa ni KWELI?
  • Si unajua siri ya kukabili  kutojisikia M-BAYA yenye mafanikio SANA inasemekana ni kujiaminisha mwenyewe KWA KUJIDANGANYA  kila mara ukijiangalia kwenye kioo kuwa WEWE MZURI?

KUJIDANGANYA ni baabu kubwa,...
... ndio maana kuna watu wengi INASEMEKANA wamefaulu mpaka KUFIKIA kuamini wataenda MBINGUNI kitu ambacho KWA MTU kunauwezekano  kikawaida na KIUDHAIFU WA KIBINADAMU  hawezi kufikia.:-(

Swali:
  • Unauhakika IMANI sio MBINU ya kumsaidia MTU KUJIDANGANYA ndio maana aaminiye N'GOMBE, mbuyu, YESU, BUDDHA, Kikwete, OBAMA , BIBI TITI, SHEKHE YAHYA , Simon KITURURU , HAWALA,  BINAMU nyama ya HAMU, wote waaminicho kwa IMANI wanakigeuza UKWELI?
NDIO,...
....kama wewe ni MTU kuna uwezekano  hicho ndicho KIPIGACHO KELELE kuwa unaweza KUDANGANYWA  .:-(

Kwanza kama utasifiwa leo kuwa UMEPENDEZA labda ni UONGO.:-(


NI WAZO TU HILI  MKUU WA KITENGO!

Hebu twende MALI  ili Mama Toumani alete mtekenyo uitwao- Niemogo

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP