Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiangalia uwezekano wa kwamba labda KUNUNA NAKO kunaambukiza!:-(

>> Thursday, March 25, 2010


Tukiachana na kununa na kumuangalia MCHUMBA MWENYE SURA MBAYA  TULIYEMPENDA KWA TABIA wakati KANUNA  anavyotufanya TUJISIKIE ,...


... labda twaweza MPAKA kustukia ,...
.... kama una-HUZUNI jaribu kujichanganya na wenye FURAHA ili uambukizwe  ANGALAU kuchekelea HATA  kanyau bila sababu.:-(





Swali:
  • SI unajua  FURAHA nayo huambukiza na ndiyo isababishayo HUWA UNASHUHUDIA  hata baadhi ya uwajuao kwa busara nao wakichekelea pia ujinga kisa wako katika mazingira ambayo komedi babu kubwa ni MTU kajamba?

  • Umefanikiwa kununa leo?
Ndio,....
..... kama unafuraha unaweza kuambukizwa KUNUNA kisa kila LIMTU likuzungukalo limenuna utafikiri kama limebanwa HAJA-kubwa   halafu aliyeko chooni anachelewa kutoka  na kuachia wengine nao starehe.ya  kupunguza  uzito MSALANI..:-(


NI HILO TU MKUU na ni wazo tu!

SIKU NJEMA Mheshimiwa!





Au hebu tumsikilize mgomvi Winnie Mandela




Au tu wa mahaba  SHAKILA arudie tu  ndude -Moyo unalia macho yanacheka

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 8:35 pm  

Leo siku nzima nilikuwa nimenuna kwa sababu ya kazi nyingi ambazo ilikuwa ni lazima nizimalize leo. Baada ya kusoma hapa nimecheka, Kununa kunaweza kuambukizwa!!!!!

Mija Shija Sayi 12:59 am  

Sidhani kama kununa kunaambukiza, labda mpaka ujue wamenunia nini, kama umezungukwa na walionuna ni rahisi zaidi kuangua kicheko kwa kule tu kuangalia sura zao zilivyogeuka vituko.

Simon Kitururu 2:33 pm  

@Mkuu CHIB: :-)

@Da MIJA: Miye wala sikubishii kwa hilo Mwaya!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP