FARAGHA!
>> Saturday, March 27, 2010
[Tahadhari : Wazo limepinda!:-(]
Tatizo la FARAGHA,...
... ni kwamba hurahisisha mpaka LILE TATIZO ULIJUALO LINAMKERA MHESHIMIWA liwekwe pembeni kwa kuwa kuna FARAGHA na kufanya lile tatizo ambalo hujui mtu analo likawa ndilo LINAPEWA KIPAUMBELE ambalo ni la MHESHIMIWA kujiangalia uchi kila nafasi ikitokea kutokana na kukwazika kwake ambako HADHARANI hakujulikani,...
...kuwa MHESHIMIWA anajihisi ana uchi wenye sura mbaya kitu ambacho ndicho kimpacho MOTISHA NA nguvu ya kukivulia gwaguro ilia KUJICHUNGULIA kuliko ILE MOTISHA YA KUDAI HAKI YA MNYONGE Mheshimiwa AJULIKANAYO KUITETEA kwenye hutuba zake zisizo kuwa faragha.:-(
LAKINI uzuri wa FARAGHA,...
...ni kwamba inaweza kukufanya UTULIE na kufikiri VIZURI jinsi ya kutatua MATATIZO YAKO na hata YA DUNIA kwa kuwa haubughuziwi na WAKUDA hapo KWENYE faragha.:-(
Swali:
- Kwani unabisha kuwa kuna watu FARAGHA ZAO huzitumia zaidi kufanya vitu vyenye undugu na KUNUSA chupi zao ili kujihakikishia ni kweli mkojo wao ukivunda haunuki vibaya sana kuliko WAFIKIRIAVYO watajiinuaje KIMAISHA wakati maisha mazuri yanapendelea MAFISADI?
- Unauhakika aamuaye kuloga mtu huwa anawazia hilo FARAGHANI au katika kijiwe cha wachawi?
- Unauhakika FARAGHA yako huwa unaitumia kufanya vya faragha au unaitumia ZAIDI kuwaza maswala yenye undugu zaidi na kitu kama kati ya KITUMBUA na MAANDAZI nini ni TAMU TAMU KAMA SUKARI zaidi?
FARAGHAAAA!
NI kweli mawazo YA MTU yasingekuwa YA FARAGHA labda tungestukia MHESHIMIWA sasa hivi umuaminiye kwa ufundi wa kusali,.......SASA HIVI anafikiria kikojoleo na baada ya hapo wazo HILO ,...
....kitakacho hitimisha siku ni lile WAZO lake la kila siku la kufikiria UBWABWA na wala sio jinsi gani Tanzania itapata umeme wa kuaminika au wataunyimaje UKIMWI usinenepe kama ifikiriwavyo na wamheshimuo MHESHIMIWA wafikiriavyo ndivyo MHESHIMIWA anafikiria.:-(
HILI NI WAZO TU na halijafanyiwa utafiti wa kina kwa hiyo kifaraja unaweza kulitukania ZAIDI ya SHENZI.:-(
Hebu Matonya abadili kwa kuongelea-Spair Tairi
Diamond alainishe zaidi kwa ndude-Kamwambie
Hebu Isley Brothers waje live na kitu -Between the Sheets
Au nimuachie tu na Notorious B.I.G a sample Between the sheets na kuifanya kitu kiitwacho -Big Poppa
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
mmmmmhhh:-(
Post a Comment