Labda ni JAMII NA MAZINGIRA YAKO tu ndiyo SIRI YA urefu wa UONYESHAVYO MASIKITIKO YAKO.:-(
>> Thursday, March 04, 2010
[Tahadhari: Wazo limenuna!:-(]
Katika juhudi za MAISHANI kufupisha HUZUNI,....
....uonekanavyo UNAHUZUNI yaweza kuwa ndio moja ya yatafriwayo kuhusu wewe ni MTU wa namna gani.:-( Lakini kwa BAHATI MBAYA yaweza pia kuwa kuna walazimikao KUCHEKELEA ya huzuni HADHARANI ,....
......kwa kuwa tu JAMII inafikiri kikutiacho huzuni hakifai kuonewa HUZUNI.:-(Swali:
- Unafikiri wakati MTU kamalizia KUWA NA HUZUNI waweza kuwa ni MIONGONI MWA WAMFANYAO inabidi aongezee MAPOZI TU ya HUZUNI ili asijeonekana MTU mbaya na MAJIRANI?
KUHUSU kuhangaikia urefu wa KUONEKANA una- MASIKITIKO na katika juhudi za kufupisha za mtu HUZUNI,....
.....waweza kusababisha MTU achanganyikiwe hata MSIBANI kwa kuwa tu mategemeo ya JAMII yanataka alie wakati labda STAILI YAKE yakukabili mambo na HUZUNI haihitaji MTU ALIE MUDA HUO na yahitaji awe pekee ili kisahihi AHUZUNIKE na wala sio HADHARANI hata kama marehemu na ya marehemu HAYAJUI yanamgusaje NA kutokana na ukweli pia kuwa MAREHEMU alivyokuwa hai kutokuwa chochote muhimu kwa MTU MHUSIKA kwa hiyo ni vigumu kuitafutia mkao wa masikitiko na kujua AHUZUNIKE WAPI kinamna gani.:-(
KUHUZUNIKA hasa sehemu ambazo utahitaji michango ya watu ya MSIBA ni SANAA pia. :-(
Swali:
- AU?
Ndio narudia,...
....MOJA ya kitu ambacho JAMII hujijengea,.....
.... ni pamoja na muda AMBAO wakujuao wanajisikia faraja kukuona una HUZUNI.:-(Na kwa bahati mbaya,...
.... kuna WAHITAJIO KUKUONEA HURUMA ambao huweza kulazimisha asiye na MASIKITIKO kuonekana mnyonge na mwenye MASIKITIKO kwa kuwa HURUMA YAO inatokana na wao kujijengea,....
Ndio ,..
.... wapo watu ambao JAMII IMEWAFUNDA kuonisha utiavyo HURUMA KIMUONEKANO ndio sawa na jinsi UNAVYOHUZUNIKA na kwa kurefusha muonekano KUWA UNAMASIKITIKO basi wewe ndio kweli MTU MZURI na umepata pigo kweli kitu ambacho huwapa faraja ya KUKUHUZUNIKIA KWA KUTO KUSUASUA kisawasawa katika hata yasiyowahusu sana wao KIHUZUNI.:-(
Swali:
- Si unakumbuka kwa aliyefiwa KUCHEKELEA Msibani sio kithibitisho aliyefiwa hana HUZUNI?
- Unafikiri kwa mwenye FURAHA ni lazima ahakikishiye wengine kuwa ni mwenye FURAHA?
Ndio,...
....LABDA.....
....ni MAZINGIRA tu na jamii ikuzungukayo AMBAVYO ni SIRI ya uonyeshavyo FURAHA YAKO,....... INGAWA wajua akenuaye meno kwa kicheko,....
.... BADO sio ushahidi kuwa ACHEKAYE na kusababisha wengine nao WACHEKE PIA kuwa ni kweli ni MWENYE FURAHA.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!
Hebu Mbongeni Ngema abadili hali ya hewa hapa KIJIWENi kwa - Woza my fohloza
Au tu Mahlathini arudie- Kazet
Au tu tudie ya matumaini tu kutoka kwa SARAFINA kuwa pamoja na yote -FREEDOM is COMING
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment