Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Yakisikilizwa MALALAMIKO YA MPENDA KULA asiyependa kupika wala kuosha VYOMBO,....

>> Tuesday, March 30, 2010

.... yaweza KUSAHAULIKA kuna watu WASIOPENDA KULA pia DUNIANI.:-(

Na akisikilizwa KIDUME mpenda WANAWAKE,.....
.... kwa muda fulani UNAWEZA kusahau kuna wasenge pia DUNIANI.:-(


Swali:
  • SI unakumbuka katika kiwanja cha MPIRA WAMIGUU unaweza kusahau uwezekano wa kuwepo washabiki wa NETIBOLI hapo?Ndio,...
.... kwa kuwa WATU WENGI wanaelekea upande wa kulia USIJE TU KUSAHAU kuwa kuna AMBAO kwa makusudi yao kabisaa wanaelekea KUSHOTO ndio maana wakati una sikiliza stori za waenda MSIKITINI au KANISANI usisahau kuna waendeao UCHAWI PIA duniani.:-(

Ndio ,....
... labda APENDAYE kula ndio anaweza stukia matatizo ya KUPIKA na kuosha vyombo na KIRUKA NJIA aliye chacha ndiye atakuwa anastukia matatizo ya gesti za migombani LAKINI na wachawi yawezekana pia wana matatizo yao tu kitu ambacho ni MCHAWI tu atastukia ni hali ya hewa gani kupaa kwa ungo ni shwari zaidi DUNIANI.:-(

Ndio,...
... labda wakati unasikia MALALAMIKO ya hili kumbuka uwezekano wa kuwa kuna MATATIZO YALALAMIKIWAYO ya lile lisilo kuhusu pia hapahapa DUNIANI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(

Hebu Ray Barretto na Mongo Santamaria katika kubadili hali ya hewa kijiweni warudie - Congo Bongo

Au tu na Kofi Olomide arudie-Sylvie


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 10:28 am  

Wanaume ndio wankuaga wabishi kupika na kuosha vyombo.......

Simon Kitururu 4:43 pm  

@Dada Koero: Labda inategemea kwa kuwa nimesikia asilimia kubwa tu ya wapishi kuanzia IKULU mpaka MAHOTELINI ni wanaume!

Na hapa tusiwasahau mabachela wote WANAUME ambao wadada bado hawajajitolea kuwapa pendo la jumla ambalo husaidia mpaka ufuaji nguo kwa wengine.:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! 1:32 pm  

Duh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP