Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UHUSIANO wa UNACHO WAZA na WEWE!

>> Monday, March 22, 2010

Anachokiwaza MTU   kingekuwa ndicho pekee kitambulishacho UTU wa mtu ,...
... labda  wengine tusingeitwa WATU na WEWE.



Na ukisoma HISTORIA utastukia , HITLER aliamini mpaka WARUSI kuwa sio watu vizuri, WAJAPANI waliamini WACHINA SIO WATU, na bila kusahau AFRIKA KUSINI kuna waliohubiri mpaka makanisani kuwa WATU WEUSI sio WATU,....
.... na ukiwaza waweza kustukia ni jinsi gani misingi ya MAWAZO HAYO yawezavyo kuota mizizi ambayo chimbuko lake ni imani kuwa MIMI kwakuwa sifanani nawe basi sina uhusiano na  WEWE.



Unachowaza ,...
... labda sicho WEWE.

Lakini unachowaza,....
..... kinaweza kuwa  kinachangia  ulivyo WEWE.:-(



Swali:
  • AU?

Kwa bahati mbaya NACHO -kuwaza,....
..... pamoja na yote nijuayo yana kuhusu wewe bado nikiwazacho sio WEWE.

Labda akiwazacho mtu wakati anawaza,...
... HICHO NI WAZO tu hata kama ndicho kifanyacho ufikirie unayekabiliana naye ni sio jini au MALAIKA  na ni MTU kama WEWE.:-(

Swali:

  • Unafikiri katika tafsiri yako ya ni nini ni   MTU ni asilimia ngapi inachukuliwa na ANACHOKIWAZA katika  kukutambulisha kwako kuwa yeye ni MTU?
  • Unauhakika kionekanacho kama mtu hakitoshi kuitwa  MTU?


UKIWAZA,...
... unaweza kuanza kuamini kuna watu uwajuao ambao wala SI WATU kwa kuwa labda wawazavyo na NGEDERE  wawazavyo ni sawa.:-(

UKIWAZA,...
... waweza mpaka kuamini kuna BATA wanafikiria kama KUKU kama kipimo ni mwendo wao wakuvuka barabara wakati wanalikimbia gari lako kwa spidi sawa.:-(

Swali:
  • Unauhakika unachowaza sio kikufanyacho  WEWE ni wewe au unafikiria ni sura lako zuri ndilo linauzito zaidi kuwa wewe ni WEWE?
  • Unafikiri SURA LAKO halinamchango fulani katika UNAVYOWAZA ?
  • Unauhakika sura yako haichangii unavyowazia MAHARAGE?

NIMEACHA na hili NI WAZO TU!


Hebu USTADHI Zakir Hussein atupigie-Tabla solo





Au tu turudi Msumbiji Mariza abadili kwa ndude-Barco Negro




Mariza alete pia - Oh gente da minha terra


Au tuamie tena Cape Verde ili LURA amwage kitu-Na ri NA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 6:34 am  

MAWAZONI nako kuna mawazo. na labda kuwaza tu hakutoshi inabidi kutumika nyezo fulani ya kibandiko bin kibandikio.

sasa tatizo ni kile tuwazacho......kwamba wengine wanafikiriaje ninapowaza????

wanajua niwazacho?

Yasinta Ngonyani 2:53 pm  

Mawazo:-( Mawazo ni nini? na kwanini watu wanawaza? Je unapowaza unawaza toka ubongoni au?Nawaza tu:-)

Simon Kitururu 1:38 pm  

@Mkuu Markus +Da Yasinta: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP