Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati mtu ANAHISI ANAKUJUA labda ndio huwa rahisi kukutukania KIPENGELE CHA SIRI AU ukiheshimucho ZAIDI YA shenzi!:-(

>> Monday, March 15, 2010

KUHISI nishai kwa kuwa WATU,...
.....huchanganya HISIA  na ni nini ni KWELI.:-(

NA kwa kuwa  kujua UKWELI ni shughuli na WATU ni wavivu kujishughulisha hasa na MAGUMU ya watu ,...
.... wapendayo kuyaamini  kirahisi hutokana na HISIA tu na labda hasa zile zimuunganishazo mtu na MAMBO YA AJABU KIMPINDO  au MAZURI KUPITA  KIASI kama SIO MABAYA KUPITA KIASI  yenye stori tamu ZITEKENYAZO HISIA KINAMNA  ingawa hayana UKWELI.:-(


Swali:
  • Huwa unakumbuka kutofautisha unavyomuhisi ASKOFU au SHEKHE na halihalisi AMBAYO ndio  ukweli ambao unaweza kuwa HUYO ni MWIZI na malaya kwa mbaaali kitu kisichokuwa na uhusiano na wadhifa wake wa DINI UUHESHIMUO ufanyao UMHISI na yeye  vingine ?

  • Si unakumbuka kama UNAHISI tendo hilo linatonya kuwa kuna kitu HUNA UHAKIKA kwa kuwa HUJADAKA MTU AKISHUGHULIKA  na labda ndio kisa bado KUNA MTU  hajamfukuza kazi hausigeli LEO  ingawa anawasiwasi ni kiburudisho cha mmewe akiwa kazini?

  • Unauhakika HUWA unajua UKWELI au hata uwaitao MAFISADI ni kwa HISIA tu ?



Na kwa KUHISI kuna wengi wanahukumu watu na VITU ,...
.... ingawa UKWELI wenyewe labda  ni kweli BIKIRA Maria baada ya kujifungua alibakia bikira  HATA KAMA hisia zako ZINAPINGA na TANZANIA kweli ina amani  kama tu isivyo UKWELI.:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Hivi hapa kwenye BLOGU huwa unahisi UNANIELEWA au unajua HUNIELEWI?


NDIO,....
....labda sio hisia zako tu,....
... kuna uwezekano UKWELI wenyewe nilichoandika ni UJINGA hapa.:-(


Lakini SI UNAJUA kama unahisi una NJAA ,....
...kumbuka wewe hunanjaa KIKWELI  kwa kuwa kwa kawaida MWENYE NJAA hujua  na sio HUHISI kuwa ANA NJAA.:-(


NIMEACHA!:-(





Hebu twende ETHIOPIA ili TEDDY AFRO arudishe mambo mpwito kwa ndude- AYNE



Au tu TEDDY AFRO atulize manyanga kwa kitu-MUZIQA HIWETE



Au tusiondoke ETHIOPIA bila TEDDY AFRO kumwaga tena ndude-JAH

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP