Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DUNIANI- katika KUFIKIRIA YA YULE anayechaguliwa KUKUMBUKWA na WANADUNIA!:-(

>> Thursday, March 04, 2010

 [Tahadhari : Wazo limenuna a.k.a HALICHEKELEI kanyau!:-(]


Binadamu wanaweza kuchagua kumkumbuka MTU kwa SURA NZURI,...
....hata kama SURA ya mtu huyohuyo  WAIPENDELEAYO KUIKUMBUKA ni sura ya kwenye PICHA za UJANANI wakati KIGOLI hajavunja ungo na bado anasura ya mduara nyeusi na KATIKA MASWALA ya uzuri hajachonga kidevu kama Michael Jackson na pia   kuanza kujichubua.

Ndio,....
.....kuna waamuao kukukumbuka kwa MAZURI,....
.... kama vile kwa kuficha MABAYA katika KUMBUKUMBU yanageuza ukweli kuwa KIJEBA kuna muda na mengi tu alikuwa anatibua.


Swali:
  • Kwani hujastukia hata waliowahi kuwa wapenzi kuamua wakumbukalo ni yale tu mabaya katika penzi lao ambayo yamesababisha katika ndoa WAMEACHANA?
  • Si unakumbuka kumbukumbu zilivyo nyoko kiasi kwamba labda MSIBA WA MWAKA JUZI  kuna mtu KIRAHISI ambaye kasahau aliyefariki ALIKUWA ni nani lakini anakumbuka MENYU aka MSOSI na charanga zake ,-  kuwa pilau lilikuwa lina bonge za nyama ya nguvu, MAJI YAKUNAWA YALIKUWA MACHAFU  na kachumbari haikuwa ya kutosha?
  • Unafikiri ni nini kinakujengea ukumbukayo?

Katika MARAISI wa Tanzania,....
..... na haki ya nani idadi yao ni KIDUCHU,...
.....lakini kirahisi kuna ambaye kama sio NYERERE  inahitaji ufikirie ni nini alichofanya  usichokikumbuka ambacho NACHO hushindwa kukukumbusha jina lake na wahitaji msaada wa GOOGLE SEARCH  ili KUMKUMBUKA.:-(

Ndio,...
...katika DUNIA kuna VIONGOZI  wengi,....
..... lakini labda ni SADDAM HUSEIN na sio WAZIRI MKUU  Sir John MAJOR  wala MSUYA  katika  ambao kirahisi  unawakumbuka.

Na taka usitake kuna NDUGU zako,....
...... ambao huwakumbuki hata wakati unajaribu NDUGU kuwakumbuka!:-(


Swali:

  • AU?
  • Unauhakika KATIKA NDUGU  ni asilimia ngapi ya NDUGU ZAKO ambao kwa jina unawakumbuka?
  • Si unajua inaweza ikawa mtihani mkubwa kwa yeyote yule ukimuuliza akutajie jina la Mjomba wa BABU yake  ukizingatia tayari shangazi ya BIBI na shoga zake waliokuwa wanacheza kujipikilisha kwa wengi kuwafahamu haileti maana?:-(


Labda  MTU huchagua  anaowakumbuka,....
.... na kunauwezekano KATIKA BINADAMU kwa  asilimia kubwa ya watu mwisho wa kukumbukwa  ni KIZAZI CHA WAJUKUU ZAO tu ambao kuna kitu kuhusu wao wanakikumbuka.:-(




Ndio,...
.... na kwa UMKUMBUKAYE  labda unachagua cha kukumbuka,....
..... na KIRAHISI baada ya muda unaweza kukuta NELSON MANDELA anakumbukwa kwa mazuri tu ingawa amekiri mwenyewe alishawahi hata kuiba udogoni na NYERERE atakumbukwa kwa yote MAZURI wakati kwa SADDAM HUSSEIN na IDDI AMINI  yaweza kuwa ni rahisi kukumbukwa kwa MABAYA TU ingawa taka usitake kuna MAZURI tu lukuki waliyowahi kufanya pia.:-(


Swali:

  • Unafikiri kwa kawaida ni mambo ya aina ngapi huwa Marehemu yoyote umjuaye huwa unakumbuka wakati unajua MTU kama MTU ana mengi ndani ya MAISHA kitu kifanyacho umjuaye kama MWIZI haki ya nani kuna mtu kwake huyo ni BABA tu MPENDWA ambaye anahakikisha familia yake haifi njaa?
  • Unafikiri utakumbukwa na vizazi vingapi , kwa lipi na KWANI  unamaindi hilo?


NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na wala USIKONDE!

Hebu twende tena Angola Carlos Burity arudie - Ojala Yeya



Au tupitie tu na CONGO Papa WEMBA arudie ndude-Awa Yo Okeyi

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 6:02 pm  

Ni hulka ya kibinadamu kukumbuka yaliyo mabaya na kusahau yaliyo mazuri,mfano katika mpapenzi kama ulitendwa na ukaumia moyo, kamwe huwezi msahau huyo mtu hata kama alitenda wema zaidi ya ubaya.....

Yasinta Ngonyani 6:18 pm  

Edna umenena kweli, atendewaye ni vigumu kusahau kuliko mtenda.

Simon Kitururu 2:32 pm  

@Da EDNA +Da Yasinta: Nakubali hilo .
Lakini hamuoni kuwa hilo laweza kuwa ni udhaifu pia ambao labda unakosoro zilezile za mtu aonaye mazuri tu katika mtu na kuruka yake mabaya kikumbukumbu?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP