Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MPENZI nasogeza sikio UNIDANGANYE vizuri wakati unanichekea!:-(

>> Monday, March 08, 2010

Kabla sijaanza,....


Swali:
  • Unafikiri ni kweli nahitaji kuambiwa UKWELI kila siku  katika kutunza FARAJA zangu?

MAISHA ni mafupi na moja ya tumizi la muda KWA BAHATI MBAYA ni kuishi na UKWELI unaouma,...
.... kwa hiyo labda usinishangae nikiombea KUDANGANYWA.:-(


Lakini kwa kuwa umejifunza UONGO NDIO  unaouma ,...

....unaweza kuamua kuishi kwa kuchunguza TARALILA AKUPAZO MPENZI kwa kuwa katika MAISHA YAKO MAFUPI NA MTU tamu  UNATAKA IWE NI tamu kama katika HADITHI  na kwa kuwa umefunzwa kuchukia  UONGO tafiti zako  zinaathiri usikiliziavyo KUDANGANYWA kitu kifanyacho KUDANGANYWA ijae uongo wenye bonge la misuli hasa kwa kuwa   NI KITU ULICHOJIFUNZA KUKIKWEPA kwa kuambiwa UONGO NDIO  UNANG'ATA na  ukiusikilizia maumivu unauma,....


... kitu ambacho chaweza kuwa kimekuandaa na KUKUSAIDIA KUZIDI KUNISHANGAA  nikidai naombea KUDANGANYWA.:-(

Swali:
  • Si unakumbuka UONGO na UKWELI labda vinanguvu sawa katika kutonesha KIDONDA kama unakidonda kitoneshekacho chenye kuleta maumivu?
  • Na si unakumbuka moja ya shughuli ya WAZAZI ni KUDANGANYA WATOTO  ingawa ni kwa kisingizio kuwa ni bado WATOTO na  ukweli ni kuwa hawahitaji kujua kuwa MSHAHARA HAUTOSHI kwa hiyo kunabaadhi ya mambo  huwanunulii  kwa kuwadanganya na kwa hiyo HUO ni UKWELI ambao hawahitaji kuujua katika faraja zao za KITOTO?


Kwa hiyo MPENZI,....
.... nidanganye unanipenda SURA na sio PESA,.....
.... na wakati  UNANIDANGANYA usisahau kunichekea.:-(


MPENZI,...

....nidanganye UNASURA nzuri na LABDA usinistue kuwa UKWENI ni kwamba unasura kama PWEZA na  wanidaka kwa sura nikuonayonayo HARUSINI kwa kuwa tu imenyunyiziwa rojo zihitajizo PESA,...

... na wakati unanidanganya HILO usilie MACHOZI yawezayo loanisha ungaunga usoni mwako na kwa hilo LABDA jaribu kunichekea.:-(


Swali:
  • Si unajua LABDA unadanganywa leo WEYE MHESHIMIWA MWENYE MIAKILI ndio kisa bado UNACHEKELEA?



Ndio,...
..... kama unaamini katika UKWELI ,...
.... ni kweli LABDA uongo nao unanafasi yake MAISHANI MWAKO  katika kukuchagulia lini UTANUNA.:-(


Na  ni KWELI,...
....unaweza kuchagua kuchekelea porojo HATA CHUMBANI na sio tu KIJIWENI kama unajua JAMAA LINADANGANYA,...
....badala ya KUNUNA.:-(



NI wazo tu HILI MKUBWA na  usikonde!


Ngojea SHIHAN abadili tena kwa ndude- SICK & TIRED




Au hebu tumpate tena Maestro DEKULA KAHANGA VUMBI katika -Bamakonde



Au tu MAKASSY arudie ndude- MAMBO BADO

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP