Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunafikiria HISTORIA ya JINSI mtu anavyojifunza kuona AIBU kukaa uchi !

>> Monday, March 15, 2010

[Tahadhari :WAZO limepinda na laweza lisikufunze kitu kama sio MFIKIRIAJI!:-(]


Mtu akizaliwa kwa taratibu huanza kujifunza,...
..... MPAKA nini kiko  UCHI,...
.... na kwa kuigiliza hufikia mpaka kutafutia titi SIDILIA.

Mwalimu mkubwa katika swala LA KUFICHA PIA mtu  ana-FUNZA,....
..... ni MACHO YA WATU na masura yao yageukavyo NAKUKUANGALIA VIBAYA wakati yanashuhudia unavyokatambuga  huku miguu iko SAA TISA KASOROBO wakati sio riadha UNAKIMBIA.:-(

Macho ya watu hata kabla HUJAKEMEWA ubane miguu watu kwa bahati mbaya wasikuone NANIHII  ndio yanafunza,....
..... kuwa kuna vitu  onyesha MIJUSI na BATA  lakini sio WATU kama  heshima yako wataka kukuanayo ifanane na jinsi JAMII yako iaminicho ni heshima ukue vilivyo UKIISHIKILIA.:-(


Swali:
  • Lakini si  unajua labda MACHONI mwa PAKA hakuna BINADAMU apendezaye UCHI?
  • Si unakumbuka ulizaliwa uchi na labda ulisha wahi kumnyea mgeni pia BILA AIBUB ingawa hilo hukumbuki?

CHA kusikitisha ni kwamba,....
.....BINADAMU kimchekeshacho utotoni kutokana na udhaifu WAKUJIFUNZA ,....
.... mpe muda waweza kumkuta HUYOHUYO kimwana UKUBWANI kilekile eti kinamfanya ANALIA.:-(


Na LABDA binadamu badala ya kuona AIBU baada ya uchi  KUJIFUNZA,.....
... angeweza kustukia katika MWILI wa binadamu  labda UCHI ni  kipengele ambacho ukijua KUKABILIANA NACHO  kinakufundisha maisha kama hasa ukikumbuka kuwa UKIJISWAFI kipengele hutanuka na shughuli ya KUJISWAFI hata uchoke inahitaji kukumbukwa kwa KUACHA UVIVU kama wataka  kipengele kivutie na wataka MWILI mzima usinuke hata kama nia sio watu wasistukie  UNANUKIA.

Na baada ya hilo la uchi  KUJIFUNZA,....
.... waweza kugundua wewe kama BINADAMU hata YAKO DHAMIRA au tu AKILI kama tu uchi unahitaji KUISWAFI mara kwa mara hata kama UNASIKIA UVIVU ili  kuwa safi kama BINADAMU kiroho na KIMWILI  na HASA kama wataka YAKUZINGUAYO uyatoke baruti na kuyapa MKIA.



Swali
  • AU?

Na kunauwezekano,...
....KUONEA aibu kitu ni kitendo cha KUJIFUNZA,...
..... na wote wachezao MUZIKI na nguo wakifuatilia HISTORIA YA WACHEZA MUZIKI  wanaweza kugundua labda starehe halisi hata ya SINDIMBA ni kuicheza titi nje kwa kuwa labda vazi halisi la kuchezea muziki wala hata sio KIBWAYA bali ni kucheza uchi.:-(



Swali:
  • Si unakumbuka kunibishia RUKSA?


Lakini kuna waaminio kutokana na mafundisho ya DINI ZAO  kuwa EVA yule demu wa ADAMU kama baadhi ya VITABU vya BAADHI YA DINI VIDAIVYO  ndiye alianzisha mchezo wa kuona AIBU na kuficha uchi baada ya kula TUNDA alilopewa na MJANJA shetani ambalo alifanikiwa kumuonjesha ADAMU  akasikia tamu ndio mpaka akajistukia yuko UCHI.

Na kama unaami HILO miye  SIKUBISHII  hasa kama umewahi KUFIKIRIA  jinsi ulivyojifunza kuwa na AIBU kukaa UCHI na kufikia hitimisho ni kosa la EVA ndio sababu unaficha uchi.:-(


Na labda PIA  ni kweli ,...
....katika HISTORIA fupi ya binadamu CHA KUSIKITISHA  huwa inaambatanisha KUZALIWA uchi  na mwisho kufa na kuoza mpaka uchi.:-(



SAMAHANI NAACHA WAZO MHESHIMIWA !:-(




Hebu tu PAPA WEMBA apoze shughuli NA KURUDISHA USTAARABU hapa KIJIWENI  kwa ndude-YOLELE


Au tu tubaki hapahapa KONGO Papa WEMBA asawazishe shughuli kwa kitu- SHOW ME THE WAY

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP