Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MIPAKA iwekwayo na UHESHIMIWA!

>> Tuesday, March 30, 2010

Kwa kuwa jamii ndio inaweka MIPAKA ya nini kisemwe,....
..... WAHESHIMIWA ndio wafao kisabuni kwa kuwa KIHESHIMA kiwakeracho wamejifunza kuwa huwa hakisemwi hadharani.:-(

Ili kisichozoeleka kisemwe,...
....yawezekana WAHESHIMIWA wajuaji inabidi waangalie upya ni nini HAKISEMWI ambacho KINAFANYIKA kwa kuwa tu jamii imeamua kiheshima hicho kitu kisiongelewe HADHARANI.:-(


Swali:
  • Si unajua kuna aliyepata mimba au UKIMWI kwa kuwa tu WAHESHIMIWA hawaongelei ngono kwa kuwa HAWATAKI KUDAKWA wakiongelea waaminicho sio tpiki ya kiheshima hadharani?

  • Hujawahi kuuonea wivu UHURU wa mtu apendaye kukusimulia ufikiriavyo ni vitu vya FARAGHA ambavyo wewe unavionea aibu mkiwa hadharani?


MIPAKA iwekwayo na HESHIMA,....
....kwa bahati mbaya inategemea mtu na mtu na ukiheshimucho kwa mtu mwingine wala HAKINA HESHIMA.:-(


Ndio ,...
.... kuna viheshimiwavyo kama tu TISHU CHOONI ambavyo hata TISHU IHESHIMIWEJE bado tumizi lake lisaidialo kuongezea heshima ya mtu hubakia ileile ya baada ya shughuli nzito TISHU ndio itakayogeuzwa kichambio.:-(

Swali:
  • Si unafahamu TISHU nayo inaheshima zake za kimakokoneo?



Hebu Erykah Badu abadili kwa kitu- Window Seat


Erykah Badu arudie ndude - Didn't Cha Know



Au tu Outkast na Slick Rick walete tena ndude- Da Art Of Storytellin

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP