Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwanini ?: -(

>> Friday, March 19, 2010


[Tahadhari: Katika wazo LILILOPINDA KWA WAVIVU WAKUFIKIRIA bado taralila ina neno CHUPI.:-(]



.......WAKATI  kuna  MPENDA KEKI alazimikaye  KUGIDA MIHOGO wakati  wengine  kwa hiari yao  WENYEWE hawaonji wagawiwazo KEKI  kwakuwa wanasubiria MIHOGO,...
....yaweza kumtungishia  MTU MIMBA ya swali;...
....``KWANINI?´´:-(


Swali:
  • AU?

Ndio ,...
...KWANINI ,...
....ni SWALI la kawaida la  mtu!:-(




Swali:

  • Unabisha?



KWANINI katika taralila yaweza kuwa  ,...
....katika chupi YA KITABIA  ivaliwayo siku ya MTU kupania kumuonjesha MCHUMBA  utupu kwa mara ya kwanza  ,...
...chupi HUWA imepaniwa iwe SAFI ZAIDI ya siku ambayo MCHUMBA HATA ANGALAU  kwa mbali hatapewa nafasi ya kukodolea uwezekano wa ``MPENZI hajavaa KIFICHA NYETI ´´  kistaarabu ,... na labda NDIYO kiashiriacho  kuwa MSTAARABU HUTAKIWI KUJUA kunasiku  mtoto mzuri  UMJUAYE KWA USAFI  labda chupi yake sio safi sana kama KIBANGA ALIYEMPIGA MKOLONI ,...

.... NA inaweza HILO  kuwa ndilo  SWALI  la MTU!:-(

NA kwanini,......
....msibani AU HARUSINI  kuna wahisio PILAU HUNUKIA  vizuri zaidi kuliko KWA MAMA NTILIE YULEYULE ambaye  ndiye aliyekuwa na TENDA MSIBANI na PIA ZILE HARUSI KADHAA ULIZO HUDHURIA  ambazo ilibidi tu uende kwa kuwa hukuchangia  pesa hata za kujionyesha tu KWA WAPAPARIKIAO WAJIONYESHAO  kuwa wanapesa kweli kifisadi ,....
...na LABDA  hilo pia NDILO ni SWALI  la mtu!:-(




Kwanini,...
...HATA ambaye kwa kawaida ndiye MWENYE NYEGE  YA DINI  AAMINIZO ZINAPELEKA WASIO WAJANJA DUNIANI  kule MBINGUNI wakati  KUMBE  sio kila wakati HUYO NDIYE anajiamini kama ATAMKIAVYO WASIOJIAMINI  hasa wakati atulizavyo manyanga ILI MEZA  itulie,...
....halafu ikitulia ndio mnastukia kumbe YEYE  NDIYE  yule  mtu wa MIZOGA wakati anaokoa SIKU  katika juhudi zake za wa ngono YA ufisadi,....


....ndio  laweza kugeuka kuwa ndilo  GUMU KINAMNA swali la MTU.:-(





Swali:
  • Kwa WATANZANIA unafikiri ni kwanini Mheshimiwa KIKWETE na sio Mheshimiwa PROFESA SARUNGI au Mheshimiwa RASHIDI KWAWAWA ndiye aliye tangulia kuwa MHESHIMIWA RAIS  WA TANZANIA kabla ya Waziri mkuu  MORINGE SOKOINE ?

  • Unauhakika kwanini YESU hakuwa MWANAMKE?

  • Umeshawahi kujiuliza NI KWANINI SIO kila lifanyikalo LIKUHUSULO HUWA UNAKUMBUKA kujiuliza KWANINI?


Ndio,...
....LABDA ni kweli  ,....
....KWANINI ni KIBONGE LA SWALI  ndio maana SIO rahisi KUJIULIZA
ni kwanini  inasemekana kuna  MWINGINE  aliyevulia mtu chupi mara moja tu  na akapata KITU CHENYE THAMANI YA UWAZIRI wakati kuna aliyevulia chupi  ZAIDI YA WATU WANNE NA NUSU  na kutopata  angalau  BILAURI MOJA ya UJI WA MUHOGO wa asubuhi moja.:-(


Ndio,...
...labda kuna sababu ,....
....KWANINI ,...
....ni SWALI la mtu.:-(
Swali:

  • KWANINI?
  • Tukiachana na UjingaBUSARA wa hiki KIJIWE huwa  LAKINI unakumbuka kujiuliza KWANINI mara kwa mara MAISHANI?

DUH !
NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA lakini ni wazo tu HILI MKUU !:-(

IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!

Hebu Hugh MASEKELA abadili tu kwa kutukumbusha SOUTH AFRICA katika JAZZ katika ndude- Strawberry





Tubaki tu Afrika Jimmy Dludlu aendelee TENA kujaribu kulainisha wajanja kwa ndude -Tote




Au tuhame tu na tupate ndude -Casanova kutoka katika unajisi wa   shughuli wa - Levert

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP