Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika swala la usichague MSICHANA kwa SURA NZURI wakati kashajiremba KIMSHEBEDUO!.

>> Wednesday, September 28, 2011

Ndio ,..
... yasemekana kwenye SIKUKUU  labda kila msichana ni MREMBO,...

.... sababu KUU ni  kwa kuwa KASHAJIREMBA,...
......  hasa kwa kuwa yasemekana SURA YAKE  sio uionayo ,...
.... kwa kuwa SURA yake KIKWELI  iko chini ya VIPODOZI!:-(


Swali:
  •  Si hapa unajua nimeruka MORANI wa KIMASAI?
  • Si bado nasikia kwa MIDUME lukuki MWANAMKE MZURI ni SURA NZURI  TU ile yenye kushikiliwa na BONGE la KICHWA kwenye  mwili wenye KIFUA chakutosha kimatiti , tako  ujazo wakutosha na  bila kusahau bonge la usafiri kimiguu yenye paja  mwanana- NA wala uzuri  sio TABIA?

Na siri ya kujua sura halisi ya WAREMBO wa siku hizi ambao ni fulu kujipodoa,...
....KUNAWASHAHURIO  mchungulie KIMWANA  asubuhi akiamka tu  wakati bado ananuka mdomo kwa kuwa bado hajaenda maliwatoni kujipodoa hata ndani ya MDOMO !:-(


Swali:
  • Hivi  si nasikia yasemekana kuna VIMWANA wazuri ambao kujipodoa ndiko kwawafanya waonekane vituko?
Samahani ni UCHOKOZI tu HUU Mwayego,...
... na wala usikonde  kama unajipodoa kwa kuwa ,...
... urembo U-jichoni mwa MTU  na kama unafikiria kwa  kujiremba kwa KUNYOA NYUSI za juu na CHINI au  hata kwa KUJICHUBUA unapendeza,...
.... basi wewe unapendeza KIGOLI  kwa kuwa MAISHA ni YAKO na JICHO ni lako wengine kama akina Simon Kitururu kwa kimbelembele chao wakidai umekaa ki sura FANTA -mwili COCACOLA  yako hayawahusu na WAKUKOME kabisaa na kimbelembele chao! 

Msuto kidogo kwa akereketwaye na kujiremba kwa mwingine :
  • LOH! Yani watuwengine bwana ,pilipili iko shamba  kibarazani kwa shoga sijui yawawashia nini?

NIMEACHA taralila hii ILIYOPINDA!


Moja kwa moja hebu tuangalie mwanadada  KOKO  ,...
...akitoa  moja ya siri katika  KUJIPODOA SURA  kwa AKINADADA katika  kusaidiao hata waopoao demu DISCO KISA ANA SURA NZURI ,...
...nini KILIFANYA  asubuhi hawana uhakika kuwa  kigoli aliyepo kitandani ni yuleyule aliyeopolewa KLABU usiku  kwa ajili ya dhambi ya chapuchapu ya ZINAA ,....

...katika :Foundation Tut/Review: feat Mac Match Master Foundation


6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:23 pm  

Wanawake/wasichana tuna kaaaaziii kwelikweliii...HONGERA KWA WAJIPODOAO..WENGINE TUKIJARIBU NI BONGE LA MCHOZI LINATOKA...SIJUI USHAMBA:-)

Rachel Siwa 7:14 pm  

kwikwikwikwikwi da'Yasinta!!kama kengere ya kanisani inagonga wewe ndiyo unaanza mpaka ibada itaisha na watu watarudi, watapika, watakula wewe hujamaliza kujipodoa, hapo usoni kaongeza kama kilo ya uzito, Mmmm Wanawake na ulembo.

Yasinta Ngonyani 8:28 pm  

Halafu Recho unajua nimewahi kujaribu weee bwana we nikajisikia uso unakunjamana kma nini mbona nilinawa maji...mie huko nimeacha kabisa kwani sipungukiwi kitu..na pia zile pesa za vipodozi nanunua kitu kingine cha maaana....MJANJA eeeehhh:-)

Rachel Siwa 8:39 pm  

Hahahahhha hebu nipe picha ulivyojiremba hukupiga?bora da'Yasinta kuacha mwenzangu si kila kiingiacho mjini tunakiweza wangu,pesa kula Matunda na wanangu dada, yaani leo umenichekesha dada na huyu kaka Simon[Mshebeduo] hayo maneno yake, wee mwache tuu akipita mitaa yao atakoma!!!!!!!

Simon Kitururu 3:50 am  

@Yasinta: Unauhakika hujirembi wewe? Maana mdada usingekuwa mke wa mtu wewee labda tungeongea mambo mengine!:-8

@ Recho: Na mbio wewee! Nikipita mitaa kwao natoka baruti tu!:-)

Yasinta Ngonyani 11:14 am  

Bahati mbaya Recho nilikuwa na haraka ya kuyatoa maana nilijisikia kama nimepaka matope:-)

Simon usiwe na shaka nina hakika kabisa 100% kuwa sijipambi.Nikioga mie huuuuuwooooo:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP